August 02, 2018

TMRC,TIOB kutoa kozi ya mikopo ya nyumba

 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Mortgage Refinance Company (TMRC), Oscar Mgaya (kushoto), akibadilishana hati ya makubaliano na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Institute of Bankers (TIOB), Patrick Mususa, kwa ajili ya kuandaa kozi ya Mortgage Finance iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande).
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Mortgage Refinance Company (TMRC), Oscar Mgaya (kushoto), akisaini makubaliano na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Institute of Bankers (TIOB), Patrick Mususa, kwa ajili ya kuandaa kozi ya Mortgage Finance iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Institute of Bankers (TIOB), Patrick Mususa, akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa kozi ya Mortgage Finance jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Institute of Bankers (TIOB), Patrick Mususa, akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa kozi ya Mortgage Finance jijini Dar es Salaam.
 Washiriki.
 Mkutano ukiendelea.
 Washiriki.
 Mkurungezi wa Masuala ya Fedha wa Benki Kuu (BoT) Alexander Ng’winamila, akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa kozi ya Mortgage Finance jijini Dar es Salaam.
 Mkurungezi wa Masuala ya Fedha wa Benki Kuu (BoT) Alexander Ng’winamila, akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa kozi ya Mortgage Finance jijini Dar es Salaam. 
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Mortgage Refinance Company (TMRC), Oscar Mgaya, akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa kozi ya Mortgage Finance jijini Dar es Salaam.
  Mkurungezi wa Masuala ya Fedha wa Benki Kuu (BoT) Alexander Ng’winamila, akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa kozi ya Mortgage Finance jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Azania Bank akitoa mada.
  
NA MWANDISHI WETU

KATIKA kuboresha mfumo wa utoaji mikopo ya nyumba hapa nchini Taasisi ya Mikopo ya Nyumba Tanzania (TMRC) na Taasisi ya Benki Tanzania (TIOB) wamekubaliana kuanzisha kozi itakayoendeleza taaluma ya kibenki.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TMRC, Oscar Mgaya, alisema kwamba mfumo wa utoaji mikopo ya nyumba bado ni mchanga na unahitaji maboresho.
Alisema kwamba kazi ya msingi ya TMRC ni kutafuta mitaji ya muda mrefu ili kukopesha mabenki ili nayo waweze kukopesha wateja wao mikopo ya nyumba ya muda mrefu. 
Mgaya alisema, ili kutekeleza majukumu yake TMRC kama mdau muhimu katika sekta hii inalazimika pia ishiriki katika kuboresha mazingira ya mfumo mzima wa mikopo ya nyumba Tanzania.
Alisema TMRC imeboresha vyanzo vya fedha kwa kwenda kwenye soko la hisa na mitaji, ambapo watatoa mikopo ya nyumba kwa mabenki yote na taasisi za fedha Tanzania.
“Tumepunguza riba za mikopo yetu kwa mabenki na taasisi za fedha, lakini pia TMRC imeanza kushiriki katika ukuzaji na uimarishaji wa soko la hisa na mitaji kwa kutoa hati fungani kama namna ya kukusanya mitaji ya ndani ya nchi na kwa nia ya kutumia fedha hizo kukopesha mabenki,”alisema Mgaya.
 kwa ajili ya mabenki kutoa mikopo ya nyumba kwa wateja wao.  Hili litafanikiwa Zaidi kama riba za dhamana za serikali zitaendelea kushuka.
Akizungumzia kozi hiyo Mgaya alisema Maofisa wa mabenki na taasisi za fedha zaidi ya 300 wamepitia mafunzo hayo.
Alisema pamoja na ushirikiano mpya na TIOB, TMRC pia itaendelea kushirikiana na Chuo cha Benki Kuu Mwanza kuendelea kutoa kozi ya mikopo ya nyumba.
Mkurugenzi Mtendaji wa TIOB, Patrick Mususa, alisema kwamba wameamua kuandaa kozi hiyo ili kuzingatia fursa zilizopo na changamoto zinazoikabili sekta ya fedha nchini.
Aidha aliwashauri wafanyakazi wa mabenki  na taasisi za fedha kuhudhuria mafunzo ya utoaji bora wa mikopo ya nyumba.
 Mkurungezi wa Masuala ya Fedha wa Benki Kuu (BoT) Alexander Ng’winamila, alisema kwamba kozi ya masuala ya mikopo ya nyumba ni muhimu katika sekta ya kibenki.
Alisema lengo la ushirikiano huo ni kuongeza wigo wa utoaji elimu na kukamilisha lengo la uwepo wa mradi wa mfumo wa mikopo ya nyumba (HFP).

No comments:

Post a Comment

Pages