Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Juma Bwire, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya usalama kuelekea mkesha wa mwaka mpya 2019. (Picha na Datus Mahendeka).
KATIKA KUMALIZA MWAKA 2018 NA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA JESHI LA POLISI MKOA WA IRINGA TUNAPENDA KUTOA SHUKRANI ZA DHATI KWA WANANCHI KWA USHIRIKIANO MKUBWA WALIOTUPA KWA LENGO LA KUPUNGUZA MATUKIO YA UHALIFU KWENYE MKOA WETU HASA KWA SHUGHULI MBALIMBALI ZA KITAIFA ZILIZOFANYIIKA NDANI YA MKOA WETU KWA SASA KUNA AMANI NA UTULIVU.
TAKWIMU ZINAONYESHA KWA KIPINDI CHA MWEZI JANUANI HADI SEPTEMBA MWAKA 2017 MATUKIO MAKUBWA YA UHALIFU YALIKUWA 1044 LAKINI KWA MWAKA 2018 KUANZIA MWEZI JANUARI HADI SEPTEMBA TUMEFANIKIWA KUYAPUNGUZA HADI 987 AMBAYO NI SAWA NA 5.7%
MAFANIKIO HAYO YANATOKANA NA MISAKO DORIA ZA MAGARI NA MIGUU TUNAZOFANYA MARA KWA MARA, TAARIFA KUTOKA KIKOSI CHETU CHA INTELIJENSIA, USHIRIKIANO KUTOKA VIKOSI VINGINE VYA ULINZI PAMOJA NA TAARIFA KUTOKA KWA WANANCHI JUU YA UWEPO AU VIASHIRIA VYA UHALIFU.
MAFANIKIO YA OPERESHENI TULIOFANYA SEPTEMBA HADI OKTOBA KESI 13 KATI YA 14 ZILIZOFIKISHWA MAHAKAMANI ZIMEPATA MAFANIKIO NA WATUHUMIWA 20 WAMEFUNGWA NA KUTOZWA FAINI.
AIDHA, OPERESHENI HII NI ENDELEVU AMBAPO KATIKA OPERESHENI ILIYOFANYIKA NOVEMBA HADI DESEMBA 13 WATUHUMIWA 18 WAMEKAMATWA KWA MATUKIO YA UVUNJAJI, WIZI WA VIFAA LAPTOP 10, FLAT SCREEN 8, TV’ CHOGO 5, DEKI 4, SABWOOFER 5 NA CPU MOJA NA NYARA ZA SERIKALI. TUNAOMBA WANANCHI WAJITOKEZE KWA AJILI YA KUFANYA UTAMBUZI.
NAPENDA KUTOA RAI KWA WANANCHI KUWA KATIKA MKESHA WA MWAKA MPYA, JESHI LA POLISI LIMEJIPANGA KUFANYA DORIA ZA NGUVU, MISAKO KILA MTAA KWA LENGO LA KUHAKIKISHA KUNAKUWA NA AMANI, UTULIVU NA HATUTAVUMILIA UFYATUAJI WA FATAKI AU KUCHOMA MATAIRI IWE BARABARANI AU SEHEMU YOYOTE. KWANI HADI SASA TUMEPOKEA OMBI LA KUFYATUA FATAKI KUTOKA KWENYE HOTELI YA SAIVILA, HIVYO WANANCHI WASIWE NA WASIWASI PINDI WAKISIKIA MLIO.
NAENDELEA KUWAASA WANANCHI KWAMBA KAMA TULIVYOPATA USHIRIANO MWAKA 2018 TUENDELEZE USHIRIKIANIO HUO MWAKA 2019 ILI MKOA WETU UWE NA AMANI NA UTULIVU.
JUMA BWIRE MAKANYA-ACP
KAMANDA WA POLISI
No comments:
Post a Comment