Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Tawi
la Benki ya CRDB la Ruangwa, Desemba 31, 2018. Kushoto ni mkewe Mary,
wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB, Ally Hussein Laay na kulia
ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Tawi la Benki ya CRDB
la Ruangwa, Desemba 31, 2018. Kushoto ni Mkewe Mary, wapili kulia ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay, wapili kushoto
ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela na kulia ni
Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Ngandirwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Tawi la Benki ya
CRDB la Ruangwa, Desemba 31, 2018. Wengine pichani kutoka kulia ni Mke
wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB,
Ally Hussein Laay na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid
Nsekela.
Jengo la Benki ya CRDB tawi la Ruangwa ambalo lilizinduliwa na
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Desemba 31, 2018.
Waalikwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati
alipozungumza baada ya kuzindua Tawi la Benki ya CRDB la Ruangwa,
Desemba 31, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi kompyuta mpakato
Kiongozi wa Chama cha Msingi cha Umoja 2017, Omari Hassani Magoma baada
ya kuzindua tawi la Benki hiyo la Ruangwa, Desemba 31, 2018. Kompyuta
Mpakato 28 zilitolewa na Benki ya CRDB kwa Vyama vya Ushirika vya
Msingi wilayani Ruangwa. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB, Ally
Hussein Laay na watatu kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB,
Abdulmajid Nsekela.
Kiongozi wa Chama cha Msingi cha Umoja 2017 wilayani Ruangwa,
Omari Hassan Magoma akionyesha Kompyuta Mpakato aliyokabidhiwa na Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa wakati Waziri Mkuu alipozindua tawi la Benki ya
CRDB la Ruangwa, Desemba 31, 2018. Kompyuta mpakato 28 zilitolewa na
Benki ya CRDB kwa vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wilayani
Ruangwa. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Hussein
Laay na watatu kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB,
Abdulmajid Nsekela. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Ruangwa, Lindi
WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa amezindua tawi la benki ya CRDB wilayani Ruangwa
na kuushukuru uongozi wa benki hiyo kwa kuwa tawi hilo litahamasisha
ukuaji wa uchumi pamoja na kuwawezesha wananchi kujua umuhimu wa
kuhifadhi fedha zao benki.
Kadhalika,
Waziri Mkuu amesema ni vema kwa benki ya CRDB ikasogeza huduma hususan
kwa wananchi waishio katika miji mikubwa iliyo mbali na makao makuu ya
wilaya kwa kufungua ofisi za uwakala na kuwaondolea adha ya kutembea
umbali mrefu.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Desemba 31, 2018) wakati akizungumza
na wananchi wa wilaya ya Ruangwa mara baada ya kuzindua tawi la benki
ya CRDB, ambapo ametumia fursa hiyo kuwahamisha wananchi kutumia benki
kwa kuhifadhi fedha zao.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu amesema kwa sasa benki hiyo inatakiwa itoe mikopo
midogo, ya kati na mikubwa kulingana na uhitaji wa wajasiriamali ndani
ya wilaya hiyo kwa sababu mikopo itawawezesha wananchi waweze kukuza
mitaji na kujikwamua kiuchumi.
Pia
Waziri Mkuu ameipongeza benki ya CRDB kwa kumuunga mkono Rais Dkt. John
Magufuli katika kuboresha maendeleo ya sekta mbalimbali zikiwemo za
afya pamoja na elimu kupitia misaada mbalimbali inayotolewa na benki
hiyo nchini.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema benki
ya CRDB imekua na kupanua wigo wake wa kufikisha huduma kwa wateja na
kuunga mkono sera ya Serikali ya kuhakikisha Watanzania wengi zaidi
wanapata huduma za fedha.
Alisema
tawi hilo ni la sita katika ukanda wa Kusini mwa Tanzania, kwani tayari
wanamatawi mengine manne ambayo ni Lindi mjini, Mtwara, Masasi,
Tandahimba na tawi linayotembea katika Wilaya ya Newala. Pia wapo
katika hatua za mwisho za ujenzi wa tawi Nachingwea.
“Wilaya
hii ya Ruangwa ni kiungo muhimu sana katika uchumi wa mkoa wa Lindi na
Taifa kwa ujumla, hivyo uwepo wa mfumo rasmi wa kibenki, kupitia tawi
hili la Benki ya CRDB, utasaidia sana kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi
kwa kufungua fursa mpya.”
Mkurugenzi huyo alisema CRDB wanajivunia utendaji mzuri wa tawi hilo, kwani katika kipindicha mwaka mmoja toka limeanza kazi, limeweza kupata matokeo makubwa ya kiutendaji ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa amana ambazo zimefikia kiasi cha shilingi bilioni 1.5.
Pia jumla
ya AMCOS 12 wanachama 4,600 zimejiunga na kufungua akaunti zao hivyo
kuongeza usalama wa fedha zao. Pia jumla ya mikopo ya shilingi bilioni
1.2 imeshatolewa kwa wateja wa wilaya hiyo, ambapo shilingi milioni 409
zilitolewa katika kilimo cha korosho na ufuta, wakati shilingi milioni
790 zilitolewa kama mikopo kwa wafanyakazi na wafanyabiashara.
No comments:
Post a Comment