*Ni kuhusu vijana waliofaulu darasa la saba
Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa mkoa wa Ruvuma uhakikishe kuwa
vijana wote wanaomaliza darasa la saba kwenye kila Halmashuri za mkoa
huo wanakwenda kuanza kidato cha kwanza.
Aametoa
agizo hilo leo (Jumatano, Januari 2, 2018) wakati akizungumza na
viongozi wa mkoa wa Ruvuma baada ya kuwasili kwenye uwanja ndege wa
Songea kuanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Ruvuma.
Waziri
Mkuu amesema Halmashuri zote za mkoa huo zijikite katika kujenga
madarasa ili wanafunzi wote waliofaulu ambao wanatakiwa kwenda sekondari
waende.
Amesema
Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kwa dhati kuahakikisha kwamba
watoto wote wenye sifa za kupata elimu ya seondari wanapata elimu hiyo
kote nchini hivyo juhudi za makusudi lazima zifanywe na kila Halmashauri
ili kutimiza azma.
Akizungumzia
suala la utoro shuleni, Waziri Mkuu amesema hilo ni moja kati ya maeneo
yanayozorotesha juhudi kubwa za Serikali za kuwapatia watoto wa
Tanzania elimu katika maeneo mengi nchini na lazima viongozi wa wilaya
na mikoa wasimame imara ili kukomesha hali hiyo.
Amesema
viongozi wa ngazi zote katika mikoa na wilaya ndiyo hasa wanaoweza
kumaliza tatizo la utoro wakishirikiana kwa karibu na wanavijiji ambao
wanaishi na watoto hao na wanajua ni watoto wangapi hawaendi shule.
Hivyo,
Waziri Mkuu amewataka viongozi hao kutoa maelekezo na miongozo
itakayowabana watoto watoro pamoja na wazazi au walezi wao kwani
wanayo mamlaka na uwezo wa kuchukuwa hatua kwa mujibu wa sheria za
nchi.
Akizungumzia zao
la korosho , Waziri Mkuu amewataka viongozi wa mkoa wa Ruvuma
kuwaondolea hofu wananchi wanaolima zao hilo katika mkoa huo kwa
kuwahakikishia kwamba Serikali inazo fedha za kutosha kununua korosho
zote ziliyovunwa na wakulima.
Kuhusu
ukusanyaji wa mapato ya Serikali, Waziri Mkuu amewataka viongozi wa
mikoa na wilaya kubeba dhamana waliyopewa na Taifa ambayo ni pamoja na
kusimamia ukusanyaji mapato ya Serikali kwa kishirikiana na Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA). "Halmashauri zote na wakuu wa wilaya wasimamie
kwa dhati ukusanyuaji wa kodi."
Akiwa
mkoani Ruvuma, Waziri Mkuu kesho anatarajiwa kufungua soko la mazao la
Lilambo katika wilaya ya Songea, kufungua ghala la mazao la Mgazini na
kuweka jiwe la msini la ujenzi wa zahanati ya Luganga na kisha
kuhutubia mkutano wa hadhara.
Keshokutwa
Waziri Mkuu ataongoza kikao cha wadau wa zao la kahawa
kitakachowashirikisha pia Waziri wa Kilimo na Mrajisi wa Ushirika.
Wengine watakaoshiriki katika kikao hicho ni viongozi wa AMCOS, UNION
na viongozi wa Bodi ya kahawa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,
Christina Mndeme wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Songea
kuanza ziara ya kikazi mkoani humo, Januari 2, 2019. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu).
No comments:
Post a Comment