June 10, 2019

MBUNGE AKABIDHI VIFAA VYA UMEME NA SARUJI KUCHANGIA MIRADI YA MAENDELEO WILAYA YA MUHEZA


Katibu Mwenezi wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Taifa Edward Simbey akizungumza jana na wananchi Kijiji cha Kwebada Kata ya Kwebada wilayani Muheza wakati Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga (Chadema) Yosepher Komba
alipokwenda kukabidhi saruji na vifaa vya umeme kwa ajili ya ofisi ya serikali ya Kijiji hicho ambavyo alihaidi.

Sehemu ya Saruji iliyotolewa na Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) Mkoa wa Tanga, Yosepher Komba.
Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) Mkoa wa Tanga, Yosepher Komba, akizungumza wakati wa halfa hiyo kushoto ni Katibu Mwenezi wa Baraza la Vijana la Chama hicho Taifa(Bavicha) Edward Simbey kulia ni Mwenyekiti wa Kijiji Cha Kwabada Joseph Emanuel.

Katibu Mwenezi wa Baraza la Vijana la Chama hicho Taifa (Bavicha), Edward Simbey, akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) Mkoa wa Tanga.
Katibu Mwenezi wa Baraza la Vijana la Chama hicho Taifa (Bavicha), Edward Simbey (kushoto), akikabidhi mpira kwa ajili ya vijana kushiriki kwenye michezo kwenye Kata hiyo kushoto anayeshuhudia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (Chadema) Yosepher Komba.
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (Chadema) Yosepher Komba akichukua kero za wananchi kwenye Kata ya Kwabada wilayani Muheza.
Sehemu ya viongozi wa Chadema na wananchi wa Kata ya Kwabada wakimsikiliza Mbunge huyo.


Muheza, Tanga

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Yosepher Komba amekabidhi vifaa vya umeme na mifuko 30 ya Saruji kwa ajili ya kuchangia miradi ya maendeleo kwenye Kata ya Kwabada wilayani Muheza.

Halfa ya makabidhiano hayo ilifanyika mwishoni mwa wiki kwenye Kata hiyo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho akiwemo Katibu Mwenezi wa Baraza la Vijana la Chama hicho Taifa(Bavicha) Edward Simbey.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo Katibu huyo aliwataka viongozi wa kisiasa kutokubagua wakati wakichangia maendeleo ya wananchi kutokana na itikadi za vyama kwani hali hiyo inaweza kuwarudisha nyuma.

Alisema kuwa viongozi wa kisiasa wanajukumu la kuhakikisha wanawatumikia wananchi wao bila ya kuweka ubaguzi wa itikadi za vyama kwani kwa kufanya hivyo wanasababisha kuzorotesha maendeleo .

Akitoleo mfano mbunge huyo ambaye ni wa kuteuliwa kupitia chama hicho lakini ameweza kutoa msaada huo kwa ajili ya uwekaji wa umeme katika ofisi ya Mtendaji na saruji kwa ajili ya ujenzi wa darasa bila kujali itikadi za kisiasa kwa sababu anajua huduma zitakazotolewa zitawagusa wananchi wa vyama vyote.

Katibu huyo pia aliwataka wananchi hao kuhakikisha wanashirikiana bila kuweka ubaguzi katika utekelezaji wa miradi ambayo inagusa maslahi ya jamii yote ili kuharakishia huduma na maendeleo yao.

Akieleza namna alivyobaini changamoto hiyo na kuweza kuipatia ufumbuzi Mbunge wa viti maalum CHADEMA Yosepher Komba alisema kuwa wakati wa ziara yake ya kutekeleza majukumu ya ubunge Jimboni hamo aliweza kupita katika kata hiyo na kukutana na changamoto ya ukosefu wa umeme katika ofisi ya Kijiji pamoja na uhaba wa vyumba vya madarasa.

Kutokana na kuwepo kwa changamoto hiyo niliwahaidi kwamba nitapeleka vifaa vya umeme kwa ajili ya kuweka katika ofisi ili huduma ya umeme iweze kupatikana na wananchi waweze kupata huduma bila yavikwazo vyovyote.

Hata hivyo alisema kwamba msaada huo wa Saruji utawasaidia kuweka kufanya umaliziaji katika ofisi hiyo lakini huku akisisitiza pia umuhimu wa kumalizia chumba cha darasa ili watoto wetu waweze kusoma bila kuwepo kwa vikwazo vya namna yoyote ile.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji Cha Kwabada Joseph Emanuel alisema kuwa msaada huo itasaidia ofisi hiyo kuwa na huduma ya umeme pamoja na ukamilishaji wa darasa katika shule ya msingi Kwabada.

No comments:

Post a Comment

Pages