June 11, 2019

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUA, ASHUHUDIA AIRTEL WAKITOA SHILINGI BILIONI 3 KAMA FIDIA NA DOLA MILIONI MOJA MCHANGO BINAFSI WA MWENYEKITI WA AIRTEL

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akimuapisha Bw. Innocent Lugha Bashungwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara  Kichere Ikulu jijini Dar es Salaam Juni 10, 2019.
 A1: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Charles Kichere kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Ikulu jijini Dar es Salaam Juni 10, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Edwin Mhede kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Ikulu jijini Dar es Salaam Juni 10, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na waalikwa akishuhudia Jaji mstaafu, Harold Nsekela ambaye ni Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Utumishi wa Umma akiwalisha kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Umma Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Lugha Bashungwa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Bw. Charles Kichere na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Edwin
Mhede Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akipokea mfano wa hundi ya dola milioni moja za Kimarekani toka kwa Mwenyekiti wa Bharti Airtel Bw. Sunnil Mittal ukiwa kama mchango wake binafsi kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Uhuru, Ihumwa, Dodoma kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akipokea mfano wa hundi wa Shilingi Bilioni 3 zikiwa ni Fidia kwa serikali ya miezi mitatu kwa hesabu ya shilingi bilioni moja kwa kila mwezi ya Kampuni ya Airtel kwa  Serikali  toka kwa Mwenyekiti wa Bharti Airtel Bw. Sunnil Mittal kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubua baada ya  baada ya kuwaapisha Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Lugha Bashungwa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Bw. Charles Kichere na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Edwin Mhede na kushuhudia kupokewa shilingi bilioni 3 kama  Fidia ya kila mwezi ya kampuni ya Airtel na dola milioni moja mchango
binafsi  wa Mwenyekiti wa Bharti Airtel Bw. Sunnil Mittal kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mwenyekiti wa Bharti Airtel Bw. Sunnil Mittal kwa kutoa dola milioni moja kama mchango wake binafsi kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Uhuru, Ihumwa, Dodoma pamoja na shilingi bilioni tatu za
Fidia ya mwezi miezi mitatu kwa hesabu ya shilingi bilioni moja kila mwezi kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mwenyekiti wa Bharti Airtel Bw. Sunnil Mittal baada ya kuwaapisha Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Lugha Bashungwa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Bw. Charles Kichere na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Edwin Mhede na kushuhudia kupokewa kwa Fidia ya kila mwezi ya kampuni ya Airtel na mchango binafsi  wa Mwenyekiti wa Bharti Airtel Bw. Sunnil Mittal
kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Jumatatu Juni 10, 2019. 
PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment

Pages