June 09, 2019

WAONGOZA WATALII BORA NCHINI WAPEWA TUZO

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Dkt. Hamisi Kigwangalla akifungua hafla ya utoaji wa Tuzo za Waongoza Watalii nchini (Tanzania Tour Guides Awards 2019) kwa mwaka ,jijini Arusha.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe. Kemilembe Walter akizungumza kwa niaba ya kamati hiyo wakati wa hafla ya Utoaji wa Tuzo kwa waongoza watalii kwa mwaka 2019, jijini Arusha.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi Tuzo ya mwongoza Watalii Bora wa muda mrefu Bi. Mary Mushi kwa kufanya kazi ya  kuongoza Watalii Mlima Kilimanjaro tangu mwaka 1979.
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi tuzo ya Mwongoza Watalii Bora upande wa Wanaume, Bw. Athuman Njiku, wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa waongoza watalii jijini Arusha.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe. Kemilembe Walter akimkabidhi Bi. Alisya Sanga Tuzo ya Mwongoza Watalii Bora kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati wa hafla ya Utoaji wa Tuzo kwa Mwongoza watalii Bora wanawake mwaka 2019, jijini Arusha.
 Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Mwenyekiti wa Kamati hiyo kwa upande wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Mhe. Peter Msigwa, kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akikabidhi tuzo kwa mshindi wa Waongoza Watalii Bora wa muda mrefu kwa upande wa wanaume.
 Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili, Utalii na Mbunge wa Nungwi - Zanzibar, Mhe. Yusuf Haji Khamis kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla, akimkabidhi Tuzo ya Mwongoza Watalii Bora Bw. Gaudence Phesto kutoka kampuni ya Kuongoza watalii ya Leopord aliyeweka rekodi ya kupanda na kushuka Mlima Kilimanjaro kwa kutumia muda wa saa 8.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akiwapongeza Washindi wa Tuzo ya Waongoza Watalii Bora kwa mwaka 2019 kwa upande wa Wapagazi Wanawake. Wa pili kutoka kulia ni Jaji Mkuu wa mashindano ya Tuzo hizo Bw. Mozes Njowe kutoka Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori MWEKA.
 Majaji walioshiriki kuteua washindi wa Tuzo za waongoza Watalii kwa mwaka 2019 wakiwa katika  picha ya pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii mara baada ya utoaji wa tuzo hizo jijini Arusha.

No comments:

Post a Comment

Pages