June 09, 2019

WAZIRI NDALICHAKO AZIPONGEZA SHULE ZA FEZA KWA KUHAMASISHA MASOMO YA SAYANSI NA HISABATI

Mkurugenzi wa Shule za Feza, Ibrahim Yunus, akisoma hotuba yake wakati wa Mahafali ya Kidato cha Sita ya Shule za Sekondari za Feza Boys kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, akitoa hotuba yake wakati wa Mahafali ya 13 ya Shele za Sekondari za Feza yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere International Convention Centre.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, akitoa hotuba yake wakati wa Mahafali ya 13 ya Shele za Sekondari za Feza yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere International Convention Centre.
Baadhi ya wanafunzi wa wahitimu wa Kidato cha Sita Feza Girls. 
Meza Kuu.
Mwakilishi wa wazazi ambaye pia ni Naibu Makamu Mkuu Chuo Kikuu Mbeya, Prof. Mtui akisoma risala.
Mwakilishi wa wanafnzi wa Feza Boys akisoma risala. 
Wanafunzi wa kidato cha tatu wakitoa burudani.
Wanafunzi wa Feza Boys wakitoa burudani.
Shaban Mohamed akipokea cheti cha mwanafunzi bora katika shughuli za kijamii kutoka kwa mgeni rasmi Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako.
Mwanafunzi Bora katika Uongozi, Ifrah Gonga akipokea cheti kutoka kwa mgeni rasmi, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako.
Mwanafunzi Bora, Khalid Hussein Abdallah, akipokea cheti kutoka kwa mgeni rasmi.
Picha ya pamoja.
 Picha ya kumbukumbu.
 

Dar es Salaam, Tanzania

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, ameupongeza uongozi wa shule za Feza kwa kuhamasisha masomo ya sayansi na hesabu  kwa kuwashirikisha wanafunzi katika mashindano ya kimataifa.

Akizungumza katika mahafari ya 13 ya kidato cha sita ya shule hizo yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam Juni 8, 2019, Prof. Ndalichako amesema kuhamasisha masomo hayo ni kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli za kuipeleka Tanzania katika Uchumi wa kati  kupitia viwanda.

"Hatuwezi kufanikiwa kuwa na uchumi wa kati unaojengwa na viwanda kama hatujawekeza na kuhamasisha elimu ya  sayansi, teknolojia na ubunifu kwa  vijana wetu" amesisitiza Ndalichako.

Aidha, Prof. Ndalichako amesema serikali  inaendelea kuboresha mazingira katika vyuo vikuu ili kuwawezesha vijana wa Kitanzania wanaojiunga na vyuo hivyo kupata elimu bora.

Amewataka wanafunzi waliomaliza kidato cha sita kuitumia vyema elimu waliopata katika kushiriki masuala mbalimbali ya kimaendeleo na kijamii. Huku akiwataka  kubadilisha changamoto mbalimbali wanaziona katika jamii kuwa fursa na  kuja na njia mbalimbali za kuisaidia kuzitatua badala ya kuwa walalamikaji.

"elimu nzuri miliyopata iwasaidie kuona fursa zaidi  badala ya kuona matatizo zaidi, sehemu mnayoiona changamoto iwasaidie kuwa wabunifu katika kuleta mabadiliko katika jamii inayowazunguka" amesema Waziri Ndalichako.

Naye Mkurugenzi wa Shule za Feza Ibrahim Yunus amesema katika kuunga mkono jitihada za serikali kutoa elimu bure, shule zake zimekuwa zikitoa ufadhili katika shule za umma zinazowazunguka ambapo mpaka sasa wanafadhili wanafunzi 184 kwa kuwapatia kiasi cha shilingi 250,000 kila mmoja kwa ajili ya kununua vifaa vya kujifunzia na kujikimu.

Mwakilishi wa wazazi wa wa wanafunzi hao Prof. Mtui ambaye pia ni Naibu Makamu Mkuu Chuo Kikuu Mbeya  ameishukuru Serikali ya awamu ya tano  kwa kuweka mazingira bora  ya uwekezaji katika elimu hivyo kuwezesha vijana wa kitanzania kupata elimu bora na kwa viwango vya kimataifa.

No comments:

Post a Comment

Pages