July 13, 2019

ACT-WAZALENDO KUCHAGUANA

Na Talib Ussi, Zanzibar
Chama cha ACT-Wazalendo kinatarajia kufanya Uchaguzi wake katika ngazi mbalimbali ndani ya chama hicho kwa ajili ya kupata safu mpya ya uongozi  ya kujipanga kuelekea uchaguzi  wa Serikali za Mitaa pamoja na uchaguzi mkuu mwakani.
Akizungumza na waandishi wa habari Visiwani hapa Ofisa wa Kampeni na Chaguzi, Muhene Said Rashid, alisema chaguzi hizo zitaanza rasmin mwezi  ujao.
Alisema chama chao kina aina mbili ya chaguzi ambapo moja ni ile katika ngazi ya Tawi, Jimbo, Mkoa na Taifa pamoja na chaguzi za Ngome zake.
Alifahamisha kuwa chama hicho kina ngome tatu ambazo ni Ngome ya Wanawake, Ngome ya Vijana na Ngome ya Wazee.
Alieleza kuwa chaguzi zote mbili zitaanza kwa kuchukua fomu na kurejesha kuazia tarehe 9-15 Agosti mwaka huu  kwa kuogombea nafasi za matawi na tarehe 19-25  August ni uchaguzi wa matawi.
Pia alieleza kuwa kuazia Tarehe 30 August hadi 05 September  2019 uchaguzi ngazi za Jimbo na Uchaguzi wa ngazi ya Mkoa iinatarajiwa kufanyika  tarehe 10 hadi 15 September  mwaka huu.
“Baada ya kukamilika chaguzi hizo awali baadae kamati kuu itakaa na kutoa taarifa ya chaguzi ngome pamoja na Uchaguzi mkuu ndani ya chama ambao utakamilika mwaka huu” alieleza Muhene.
Ikumbukwe chama hicho kilifanya uchaguzi wake wa mwanzo mwaka 2014 na kwa mujibu wa Muhene chama hicho kinalazimika kufanya uchaguzi  ili kutimiza matakwa ya sheria za vyama vya siasa nchini.

No comments:

Post a Comment

Pages