July 12, 2019

LG yaingiza mashine inayotoa uchafu wa nguo pasipo kufuliwa

 Janeth Jovin 

Kampuni ya LG kwa kushirikiana na Kampuni ya Mohammed Interprises Tanzania (MeTL) imeingiza nchini mashine inayotoa uchafu, bakteria, virusi na harufu mbaya katika nguo bila kufuliwa.

Mashine hiyo inayojulikana kama Styler hupunguza zaidi ya asilimia 99.9 ya virusi na bakteria zilizopatikana katika nguo na kuondoa mikunjo.

Akizungumza katika maonyesho ya bidhaa mpya zilizoingizwa katika soko la Tanzania, Mkurugenzi mkaazi wa bidhaa za LG Tanzania na Zambia, Keewook Song anasema bidhaa hizo zimeingizwa nchini ili kuwapunguzia watanzania adha ya kufua mara kwa mara na kuendana na kasi ya ukuaji wa sayansi na teknolojia.

“Kuna baadhi ya nguo ambazo hazipaswi kufuliwa mara kwa mara ili ziendelee kiwa katika hali ya kuvutia hivyo hili ni suluhisho la pekee, itatoa uchafu wote, harufu, mikunjo na hii itampunguzia mtumiaji kupoteza muda katika kunyoosha.” Anasma Song na kuongeza

Mbali na mashine hiyo pia friji pia kampuni hiyo imengiza friji yenye yenye uwezo wa kuonyesha bidhaa za ndani baada ya kugongea mara mbili mfano wa kubisha hodi katika kioo chake ili kuruhusu taa ziwake, viyoyozi vya kusimamisha sakafuni, televisheni pamoja na spika.

Pia imeingiza mashine ya kufulia ili na milango miwili na inaweza kufanya kazi kwa wakati mmoja, kiyoyozi cha kusimamishe sakafuni.

Mkurugenzi wa masoko kutoka (MeTL), Fatema Dewji anasema kutokana na kutambua uhitaji wa watu katika kutumia bidhaa za LG wameamua kutengeneza mfumo maalumu ujulikanao kama lipa kwa awamu.

“Mfumo huu utamuwezesha mteja kuchukua bidhaa yoyote katika maduka yetu iliyo na thamani ya zaidi ya Sh1 milioni na kulipa asilimia 20 za awali na kuendelea kulipa kiasi kilichobakia katika muda wa makubaliano.” Anasema Fatema na kuongeza

“Na mpango huu utahusisha watu tofauti ambao watafanyiwa ukaguzi ili kujirishisha kabla ya kumpatia bidhaa hiyo.”

No comments:

Post a Comment

Pages