July 26, 2019

MADIWANI RUNGWE WALALAMIKA KUADIMIKA KONDOMU

Na Kenneth Ngelesi, Rungwe

MADIWANI Halmashauri ya Rungwe Mkoani wameagiza Ofisi ya Mkurugenzi kuharakisha usambazi wa mipira ya kiume ‘Kondomu” katika Vituo vya Afya, Zahanati na maeneo ya vijijini kwani imeadimini na hivyo kuhatarisha maisha ya wananchi.

Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani kilicho keti juzi Diwani Samwel Mwakasege kata ya Matwebe alisema kuwa katika kata yake huduma hiyo imeadimika hivyo anaiombo Ofisi ya Mkurugenzi ifanye haraka kusambaza mipira hiyo.

Mwakasege alisema ni vema ofisi ya mkugenzi kupitia Mganga Mkuu ikaharakisha kusambaza mipira hiyo kwani maeneo mengi hazipo na hata zikipiatikana zinauzwa kwa bei kubwa kuanzia 1500-2000 na wananchi wengi hawawezi kumudu.

‘Mwenyekiti kwenye Vituo vya Afya Zahati kondomu hakuna, niiombe  Ofisi ya Mkurugenzi iharakishe kusambaza mipira ya kiume maana watu wetu maisha yao yapo haratini zinazopatiakana zinauzwa bei kubwa na wananchi wetu hawawezi kumudu bei gharama’ alisema Mwakasege.

Akitolea ufafanuzi juu kuadimini kwa kondomu katika Zahanati na vituo vya Afya kwa niaba ya Mkugenzi wa Halmashauri, MgangaRungwe na Mganga Mkuu Wilaya, Dk John Damian Mrina alisema wamepotekea ombi suala hilo kutoka kwa Diwani na watalifanyia kazi.

Dk Mrina alisema Mipra ya kiueme ipo ya kutosha kwana mpaka Mei 7 mwaka huu kwenye ghala la dawa kuna mpira zaidi ya 50,000 hivyo wanashukuru kwa taarifa hivyo wataifanyia kazi.

‘Mwenyekiti Mzigo upo wa kutosha kwani nimewasiliana na mtu dawa kwamba mapaka jana kuna kondomuy zaidi ya 50000 hivyo niwatoe shaka wahesmiwa madiwani ommbi lao tutalitekeleza na maalia ambapo hazipo tutawasiliana na waganga wakuu katika Vituo vya Afya na Zahanati’ alisema Dk. Mrina.

Akihitimisha hoja hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri ameitaka ofisi ya Mkurugenzi kuharakisha kusambaza mipira haraka katika vituo vya Afya Zahanati,kwenye baa na vilabu vya Pombe za kienyeji ili kunusuru maisha ya wananchi.

‘Mkurugenzi naomba mfanye haraka kusambaza kondomu kwenye vituo vya Afya, Zahanati lakini kwenye vilabu vya pombe za kienyeji ndiko waliko wananchi, narudia hasa kwenye vilabu vya pombe chonde watu wetu wataangamia’alisema Mwakota.

No comments:

Post a Comment

Pages