Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
Abiria wa Kivuko cha MV Mwanza na MV Misungwi kuhusu ujenzi wa Daraja litakalopita ziwani katika eneo la Kigongo na
Busisi mkoani Mwanza. Mkandarasi wa Daraja hilo anatarajiwa kupatikana ndani ya
miezi miwili na Daraja hilo litakuwa na urefu wa kilometa tatu zitakazopita
majini. Daraja hilo litagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 300
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono
abiria wa Kivuko cha MV Mwanza na MV Misungwi mara baada ya kuzungumza nao
katika eneo la Busisi Sengerema mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kupanda
Kivuko cha MV Mwanza katika eneo la Busisi wakati akitokea Geita. PICHA NA
IKULU.
No comments:
Post a Comment