NA DENIS MLOWE, IRINGA
MASHINDANO
ya kutafuta vipaji vya kuimba yanatarajia kuanza hivi karibuni katika
kata ya Mwangata kwa vijana mbalimbali kutoka kata kuonyesha vipaji
vyao.
Akizungumza
na Tanzania Daima, Diwani wa Kata ya Mwangata, Nguvu Chengula (pichani), alisema
kuwa mashindano hayo yanatarajia kufanyika Ukumbi wa shule ya Sun
Academy ambapo amewataka vijana wa kata hiyo kujitokeza kwa wingi.
Nguvu
ambaye hivi karibuni alianzisha mashindano ya mpira ya kombe la Nguvu
na ubingwa kuchukuliwa na Isoka fc alisema kuwa mashindano hayo yana
lengo la kuibua vipaji katika kata hiyo.
Alisema
kuwa katika kata ya Mwangata kuna vipaji mbalimbali baada ya kubaini
wakati wa mashindano ya mpira na kuombwa na vijana hao kuanzisha
mashindano ya kutafuta vipaji.
"Natoa
wito kwa vijana wa kata ya Mwangata kujitokeza kwa wingi katika
mashindano haya ya kuimba kwa kuwa tumejipanga vyema na kikubwa wapige
simu kwa namba 0657497294 ambaye ni mratibu wa kutafuta vipaji" Alisema
Nguvu
alisema kuwa kata ya Mwangata hapo mwanzo ilikuwa haina mwamko katika
tasnia mbalimbali za michezo hivyo tangu awe diwani mwamko umekuwa
mkubwa kwa kutumia msemo wa yajayo yanafurahisha.
Alisema
kuwa licha ya mashindano ya kutafuta vipaji amepanga kuanzisha
mashindano mengine ya soka yatakayojulikana kwa jina la Mtaa kwa Mtaa
Challenge Cup ambayo yatashirikisha timu za mitaa yote ya Mwangata.
Nguvu
ambaye amejitokeza mmoja ya wadau ambao wameinua michezo mkoani hapa
alisema washindi wa mashindano hayo watarajie zawadi nono kuliko
zilizotolewa katika kutafuta bingwa wa kombe la Nguvu.
Katika
mashindano yaliyoisha hivi karibuni ya Nguvu Cup bingwa aliondoka na
sh. 500000,mshindi wa pili sh. 300000 na mshindi wa tatu sh. 200000.
No comments:
Post a Comment