July 30, 2019

WATAALAMU WA MAABARA WAPIGWA MSASA WA USIMAMIZI WA VIMELEA HATARISHI

Mratibu wa Afya Moja Kitaifa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka, akieleza umuhimu wa mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia kwa wataalamu wa maabara wakatia akifungua mafunzo hayo yaliyowahusisha wataalamu hao kutoka sekta ya Afya ya Binadamu na Wanyama, Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.
 
 
Na  OWM, ARUSHA
 
Wataalam wa maabara nchini kwa kutumia Dhana ya  Afya moja ambao ni wataalam wa maabara kutoka sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wameendelea kupewa mafunzo ya Msingi ya  Usimamizi na udhibiti  wa vimelea hatarishi  vya kibailojia kwa kuimarisha ulinzi na usalama wa sampuli za vimelea hivyo.
Vimelea hatarishi  vya kibailojia vinaweza sambaza magonjwa kwa wanyama na binadamu iwapo ulinzi na usalama wake hautaimarishwa wakati wa kuvichukua  kwa wanyama, binadamu na mimea  au  wakati wa kusafirisha vimelea hivyo na  kuvipeleka maabara kwa ajili ya Uchunguzi  pia wakati kuvifanyia uchunguzi pamoja na wakati wa kuviharibu mara baada ya kuvifanyia uchunguzi.
Akiongea wakati wa kufungua mafunzo hayo, leo tarehe 29, Julai, 2019,  Mratibu wa Afya Moja Kitaifa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka amefafanua kuwa Mafunzo hayo ni mwendelezo wa mafunzo ya msingi ambayo wataalam hao tayari walishafundishwa mafunzo ya awali ya Usimamizi  na Usalama wa vimelea hatarishi vya kibailojia mnamo mwezi Machi, mwaka huu.
 “Lengo la mafunzo haya ni kuiwezesha nchi yetu kuwa na wataalamu wa maabara wenye uelewa kuhusu dhana za vihatarishi vya kibaiolojia, ikiwemo wakati wa kusafirisha vimelea hivyo na  kuvipeleka maabara kwa ajili ya Uchunguzi  pia wakati kuvifanyia uchunguzi pamoja na wakati wa kuviharibu mara baada ya kuvifanyia uchunguzi” amesema Chinyuka
Wakiongea kwa nyakati tofauti washiriki wa mafunzo hayo wamebainisha kuwa baada ya mfunzo hayo, mienendo na matendo yao wakiwa  maabara itazingatia usalama wa afya zao na usalama wa jamii inayowazunguka pamoja na Usalama wa watanzania, kwa kusimamia na kudhibiti vihatarishi vya  kiulinzi na usalama vitokanavyo na vimelea hatarishi amabavyo wataalamu hao wamepewa dhamana ya kuvifanyia kazi.
Mafunzo hayo ya siku tano, yameandaliwa na DTRA na Sandia National Laboratories na wawezeshaji wa hapa nchini kutoka wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii,Jinsia , Wazee na watoto pamoja na Wizara ya Uvuvi na Mifugo, chini ya Uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu.
Afya Moja ni dhana ni dhana inayojumuisha sekta ya afya ya binadamu , wanyamapori, mifugo na  mazingira katika kujiandaa , kufuatilia  na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu ,wanyamapori na mifugo.

No comments:

Post a Comment

Pages