July 19, 2019

ZAIDI YA DOLA MILIONI 200 ZA KIMAREKANI KUTUMIKA KATIKA MRADI WA KUUNGANISHA UMEME TANZANIA NA KENYA


Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa kuunganisha umeme kati ya Kenya na nchi Tanzania.
 Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania Mkoa wa Arusha  (Tanesco ), Herrin Mhina, akitoa maelezo ya mradi mbele ya mgeni rasmi.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Murro, akizungumza katika uzinduzi huo wa mradi wa kuunganisha umeme Kenya na Tanzania.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha akioneshwa mchoro wa mradi huo na mkandarasi wa mradi wa kuunganisha umeme kenya na Tanzania  mkandarasi m/s Gopa kutoka International Enegy Consultant GmbH kutoka ujerumani.
 

Na Ahmed Mahmoud, Arusha

Zaidi ya dola za kimarekani USD 258.82 milioni zinatarajiwa  kutumika katika mradi wa kuunganisha umeme kati ya nchi za Kenya na Tanzania ,ambapo mradi huu utahusisha ujenzi wa laini kubwa ya msongo wa kilovolti 400 kutoka Singida kupitia Manyara na upande wa Arusha kwa upande wa Tanzania hadi Isinya kwa upande wa Kenya.

Akizungumza  wakati wa makabidhiano kwa mkandarasi wa ujenzi huo  meneja wa shirika la umeme Tanzania mkoa wa Arusha  (Tanesco ), Herrin Mhina, alisema kuwa mradi huu ni mkubwa wa kimkakati wa serikali  na laini hii itakuwa na urefu wa kilometa 510.7 ambapo kilometa 414.7ni kwa upande wa Tanzania yaani ya Singida na Namanga na kilometa 96 ni kwa upande wa kenya itakayo toka Namanga hadi Isinya.

Alisema sambamba na ujenzi wa laini pia mradi utahusisha upanuzi wa vituo vya kupooza umeme vya dodoma na singida pamoja ujenzi wa kituo kipya cha kupooza umeme chenye uwezo wa kilovolti 400 kinachojengwa Arusha katika kijiji cha Lemgur ,aidha pia mradi huu utahusisha usambazaji wa umeme vijijini ambapo jumla ya vijiji 22 vilivyopo kandokando ya mradi vitanufaika kwa kuunganishiwa umeme wa msongo wa 33kV vikiwemo vijiji tisa vilivyopo ndani ya mkoa wa Arusha .

Alisema kuwa malengo makuu ya mradi ni kuongeza uwezo wa kusafirisha umeme kwenye gridi yetu ya taifa kufikia kiwango cha juu cha 2000MW pia mradi huu utasaidia kuwezesha upatikanaji wa umeme wa uhakika na kwa bei nafuu kuelekea uchumi wa kati na Tanzania ya viwanda  pia mradi huu utawezesha nxhi moja kuweza kuuza umeme kwa nchi nyingine kwa bei nafuu pindi itakapotokea uhitaji hivyo kusaidia kukuza undugu na ushirikiano uliopo baina ya nchi ya kenya na Tanzania.

"mradi huu unatarajiwa kukamilika ifikapo april 2020 ambapo gharama za mradi zimekadiriwa kuwa USD 258.82milioni kati ya hizo USD 214.93ni fedha za mkopo toka AfDB na JICA na USD 43.89 milioni zikiwa ni fedha kutoka ndani"alisema Mhina

Akizindua rasmi ujenzi wa mradi huo mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alipongeza serikali kwa kuwaletea mradi  huu kwani  huu utachangia kuimarisha uwezo wa usambazaji wa umeme kwa wananchi na katika nchi zote mbili na katika eneo la Afrika mashariki kwa ujumla pia zitasaidia kuondoa baadhi ya gharama za uzalishaji wa umeme wa kutumia mafuta mazito na gesi kwa kutumia umeme wa maji ambayo itasaidia kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa.

Alibainisha kuwa  mradi huu pia umekuja na faida kwani umepita katika kijiji cha  Lemgur na umewasaidia wananchi hao kupata umeme wa uhakika pia  wananchi wa kijiji hicho watanufaika na barabara ambayo ni sehemu ya ujenzi wa kituo cha kupooza umeme pia mradi huu utasaidia kuondoa changamoto kubwa ambayo ilikuwa inawakabili wananchi wa eneo hili,na waanchi wa wote ambao awana umeme watapata. 

Msipeane umeme kwa urafiki,wala kujuana tutafatilia ugawaji wa umeme huu na umeme huu usitolewe kwa kujuana maana huu mradi ni kwaajili ya wananchi"alisema Gambo

Aliwasihi wananchi kuacha nafasi ya kupitisha barabara na mitaro ili shughuli za maendeleo ziweze kuja kwa urahisi kwani kukiwa na barabara ni rahisi shughuli za maendeleo kufanyika kiurahisi .

Nae mkuu wawilaya ya Arumeru Jerry Muro alitumia mda huo kuwaomba wakandarasi hao kuwapatia vijana wa eneo hilo ajira vijana kwani kuna vijana wengi wa eneo hilo wenye nguvu na weledi aidha aliwasihi vijana wa eneo hilo iwapo watapatiwa ajira wafanye kazi kwa nizamu ,weledi,na wasiwe wadokozi kwani iwapo kijana yoyote ataajiriwa alafu akafanya udokozi au utovu wa nithamu wa aina yoyote hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Naye mkandarasi wa mradi huo  mkandarasi m/s Gopa kutoka International Enegy Consultant GmbH kutoka ujerumani alisema katika mradi huo changamoto inayowakabili ipo katika ujenzi wa barabara ambapo usanifu wa barabara ulilenga kuwa na barabara yenye viwango sawa na barabara za TARURA ambazo zinaupana  usiopungua mita 15  kutoka katika barabara hivyo kuwezesha kuwepo na mitaro ya maji ambayo sio muhimu tu kwakuilinda barabara balilakini pia kuzuia maji kufikakwenye makazi ya watu .

"Atukuweza kupata eneo la kutosha kwa kuwa sehemu nyingi wananchi wamejenga uziomashamba na hata nyumba ,hivyo changamoto kubwa ni kupata eneo la kujenga  mitaro ya maji yenye kukithi usanifu wa awali" .

No comments:

Post a Comment

Pages