August 03, 2019

CRDB YAZINDUA ZAO JIPYA LA SAFARI LOAN

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Adolf Mkenda, akimkabidhi ufunguo wa gari jipya Mkurugenzi wa Kampuni ya Excelent Guides Diason baada ya kupata mkopo wa CRDB wa zao jipya la SAFARI CAR LOAN uliozinduliwa jijini Arusha.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania Jaji mstaafu, Thomas Mihayo, akimkabidhi ufunguo wa gari Jipya Mkurugenzi wa Kampuni ya Nature Responsible Safari, Bi Francisca Masika, ambaye ni mwanamke pekee aliyenufaika na mkopo wa benki ya CRDB wa zao jipya la SAFARI CAR LOAN uliozinduliwa leo jijini Arusha.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.  Adolf Mkenda , akimkabidhi ufunguo wa gari mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Samless Adventures Sam Manonga baada ya kupata mkopo kutoka benki ya CRDB katika halfa ya uzinduzi wa zao jipya la SAFARI CAR LOAN unaotolewa na benki ya CRDB.

  
 Na Mwandishi Wetu

Katika kuunga mkono jitihada za serikali za kukuza sekta ya utalii nchini benki ya CRDB imezindua zao jipya la kibiashara liitwalo “SAFARI CAR LOAN”zao ambalo lina lengo la kuwawezesha wajasiriamali waliopo katika sekta hiyo kufanya biashara yao kwa ufanisi kwa kuwapatia mikopo ya magari mapya ya utalii kwa riba nafuu .

Mkopo huo wenye riba ya asilimia 10 unatolewa na benki ya CRDB ambayo imeingia mkataba na kampuni ya utengenezaji magari maalum ya utalii ya Hanspaul ya jijini Arusha ambayo gari jipya hugharimu kiasi cha dola elfu sabini na tano hadi laki moja ambayo mkopaji atarejesha mkopo ndani ya miaka mitano.

Afisa Biashara Mkuu wa Benki ya CRDB, Dk. Joseph witts akizungumza hafla maalum ya uzinduzi wa zao hilo la Safari Car Loan jijini Arusha iliyoenda sambamba na kongamano la utalii liloshirikisha a wafanyabiashara kutoka Hongkong China ,Tanzania na taasisi za serikali zinazojihusisha na uwekezaji dakta Witts alisema lengo la kuanzisha zao hilo ni kutatua changamoto ya usafiri usafiri katika sekta hiyo.

“CRDB tumekuja kutatua changamoto kubwa ambayo wafanyabiashara wamekuwa wakikumbana nayo kutokana na ukosefu wa mitaji ya kuweza kununua magari ya kusafirishia watalii tukijua kwamba utalii unachangia sehemu kubwa katika pato la taifa”alisema Witts.

Kwa upande wake Katibu mkuu wizara ya maliasili na utalii profesa Adolf Mkenda aliipongeza benki ya CRDB kwa uvumbuzi wa zao jipya la kibenki ambalo litasaidia wajasiriamali kuweza kujipatia magari ya kusafirisha watalii kwa uhakika Zaidi.

“Uvumbuzi huu wa zao jipya la biashara la kibenk linasaidia wajasiriamali kuweza kujipatia magari ya kubeba watalii, huu ni ubunifu mzuri utasaidia vijana wetu ambao hawana mitaji mingi kuweza kujiingiza kwenye shughuli hizi hususani wakati huu ambao serikali ikiiendelea kuongeza vivutio vya utalii nchi”alisema Mkenda.

Kwa pande wao baadhi ya wanufaika wa mikopo hiyo bi Fransisca Masika mkurugenzi wa kampuni ya Nature Rensiposible Safari na Sm Mwanonga mkurugenzi wa kampuni ya SAMLESS Adventures wameishukuru CRDB kwa mkopo huo ambao walisema utaboresha biashara yao.

No comments:

Post a Comment

Pages