Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshuhulikia Wanawake Duniani (UN WOMAN) Bibi. Hodan Addou wakati Bibi Addou alipofika
Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini Dar Es Salaam leo Agost 14,2019 kwa
ajili ya kumshukuru Makamu wa Rais kwa kuweza kuimarisha Ulizi wa Masoko kwa
kuzuwia Utumikishaji wa Wanawake na watoto Masokoni ambapo pia amesema Shirika
hilo kwa kushirikiana na Benki ya Dunia wameandaa Warsha itakayozungumzia
kuhusu Wanawake kuweza kutambua hali zao kwenye suala zima la Biashara. (Picha
na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan akisalimina na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshuhulikia Wanawake Duniani (UN WOMAN) Bibi. Hodan Addou wakati Bibi Addou alipofika
Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini Dar Es Salaam leo Agost 14,2019 kwa
ajili ya kumshukuru Makamu wa Rais kwa kuweza kuimarisha Ulizi wa Masoko kwa
kuzuwia Utumikishaji wa Wanawake na watoto Masokoni ambapo pia amesema Shirika
hilo kwa kushirikiana na Benki ya Dunia wameandaa Warsha itakayozungumzia
kuhusu Wanawake kuweza kutambua hali zao kwenye suala zima la Biashara.
Na Mwandishi Wetu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan, amelitaka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshuhulikia Wanawake
Duniani (UN WOMAN) kuandaa Tathmini ya kinchi kuhusiana na
Kongamano la Beijing.
Amesema ni Vyema kuwepo na uwezekano wa kuweza kuandaa
Tathmini ya uhakika itakayoweza kuonesha hali halisi ya Idadi ya Wanawake
waliopo katika Nafasi mbalimbali za Kiuongozi hususan kwenye Baadhi ya
Mashirika na Taasisi Binafsi.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo Agost 14, 2019 Ofisini
kwake Ikulu Jijini Dar Es Salaam wakati alipokutana na kuzungumza na Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshuhulikia Wanawake Duniani (UN
WOMAN) Bibi Hodan Addou.
Aidha Makamu wa Rais
amelishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshuhulikia Wanawake Duniani (UN WOMAN) kwa kuendelea kuweza kutoa fursa
katika nyanja mbalimbali za Kijamii na kimaendeleo kwa Wanawake Duniani na
kulitaka Shirika hilo kuendelea kuzidi kutoa fursa hizo kwa Wanawake Hususan kwenye
sekta za Kilimo.
Nae Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshuhulikia
Wanawake Duniani Bibi Hodan Addou aliyeambatana na Bw. Denis Maro Biseko
Mwakilishi wa Benki ya Dunia hapa Nchini, amemshukuru Mhe. Makamu wa Rais kwa kuweza
kuimarisha Ulizi wa Masoko kwa kuzuwia Utumikishaji wa Wanawake na watoto
Masokoni. Ambapo pia amesema Shirika hilo kwa kushirikiana na Benki ya Dunia
wameandaa Warsha itakayozungumzia kuhusu Wanawake kuweza kutambua hali zao
kwenye suala zima la Biashara.
No comments:
Post a Comment