August 04, 2019

RC SIMIYU AIPONGEZA MSD KWA KUBORESHA HUDUMA ZAKE

 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mh Anthony Mtaka akisaini katika kitabu cha wageni alipotembelea banda la Bohari ya Dawa (MSD) katika Maonyesho ya Wakulima Nanenane yanayoendelea Viwanja vya Nyakibimbi mkoani humo.
 Wafanyakazi wa MSD ambao wapo kwenye maonyesho hayo.
 Mhe.Mtaka akiwa na Wafanyakazi wa MSD katika banda lao.
 Wananchi wakiangalia kitanda cha Hospitali vinavyouzwa na MSD walipotembelea banda la MSD kwenye Maonyesho hayo.
Hapa mmoja wa wananchi akiangalia vifaa vilivyomo kwenye mfuko maalumu wenye vifaa vya kujifungulia wajawazito alipotembelea banda la MSD kwenye Maonyesho hayo.

Na Mwandishi Wetu, Simiyu

MKUU wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka, ameipongeza Bohari ya Dawa (MSD) kwa kuboresha huduma zake, hasa kwenye upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.  

Mhe. Mtaka alibainisha hayo wakati alipotembelea banda la MSD lililoko kwenye maonesho ya Nane Nane katika viwanja vya Nyakibindi Mkoani Simiyu, na kuzungumza na watendaji wa MSD wanaoshiriki maonyesho hayo.

Aidha apongeza MSD kwa kuazimia kujenga kituo cha mauzo (Sales Point) mkoani Simiyu, kwani hatua hiyo itarahisisha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba, na vitendanishi vya maabara mkoani humo na mikoa ya jirani.  

Mtaka amewakaribisha wadau mbalimbali kuwekeza mkoani Simiyu kwani mkoa huo unazo fursa nyingi za kiuchumi, ili kuinua pato la taifa na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.  

MSD inashiriki maonyesho ya Nane Nane yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya Nyakibindi mkoani Simiyu, kwa kutoa huduma za dawa na ushauri kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment

Pages