Meneja
Ukuzaji wa Biashara Kitengo cha biashara ndogondogo na za kati wa Benki ya NBC, Jonathan Bitababaje, akiwasilisha
mada kuhusiana na huduma za benki hiyo wakati wa Kongamano la kibiashara
lililoandaliwa na Benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wadogo na wa kati mkoani
Dodoma lilillofanyika hivi karibuni jijini humo.
Dodoma, Tanzania
Benki
ya NBC imeratibu kongamano maalum la kibiashara kwa ajili ya wateja wake wadogo
na wakati jijini Dodoma ambalo pamoja na mambo mengine lililenga kuwaongezea
wateja hao hao uelewa kuhusiana na mabadiliko ya kihuduma na fursa za
kiuwezeshaji kutoka benki hiyo.
Akizungumza
wakati wa kongamano hilo lililofanyika hivi karibuni jijini humo, Meneja Ukuzaji wa Biashara
Kitengo cha biashara ndogondogo na za kati wa Benki hiyo, Bw Jonathan Bitababaje alisema kufuatia
uboreshwaji mkubwa wa huduma za benki hiyo ambazo zinaendana na kasi ya kiteknolojia
na fursa za kiuchumi kumekuwa na hitaji kubwa kwa wateja hao kujengewa uelewa
ili waweze kwenda sambamba na mabadiliko hayo.
“NBC
kwasasa tumefanya mabadiliko makubwa ya kihuduma yanayoendana na kasi ya
kiteknolojia na ukuaji wa uchumi na tumeona kuwa mabadiliko haya yatakuwa na
tija zaidi kwa wateja wetu hasa wadogo na wakati ikiwa tu tutawajengea uelewa wa kutosha ili
waweze kwenda sambamba mabadiliko haya badala ya kuwa changamoto,’’
alibainisha.
Alisema
mbali na kuwajengea uelewa kuhusu huduma za benki hiyo,kupitia kongamano hilo
washiriki waliweza kutoa maoni yao ikiwa ni mrejesho wa huduma wanazopata
kutoka benki hiyo, hatua aliyosema itasaidia taasisi hiyo kuboresha zaidi huduma hizo sambamba na kubuni
huduma mpya zinazoendana na mahitaji ya wateja hao.
Aidha
katika kongamano hilo la siku moja, mbali na masuala ya kibenki washiriki
walipata fursa ya kusikiliza na kuchangia mada kutoka kwa wawakilishi wa
taasisi nyingine ikiwemo Chemba ya biashara, viwanda na kilimo (TCCIA)na Baraza la Uwezeshaji (NEEC) ambao walielezea
fursa mbalimbali za kibiashara ndani na nje ya nchi ikiwemo nafasi ya taasisi
hizo katika kuwaunganisha wafanyabiashara na wenzao kutoka nje ya nchi.
“
Kwa kushirikiana na benki ya NBC tumekuwa tukishirikiana mambo mengi
yanayolenga kuwasaidia wafanyabiashara wetu na hivi karibuni tunatarajia
kuwasafirisha wafanyabiashara kwenda nchini China kwa ajili ya safari ya
kibiashara ya siku kumi ambapo wahusika watalipa gharama ya kiasi cha Dola za
Kimarekani 2500 tu ambayo itagharamia mahitaji yao yote ya msingi ikiwemo nauli
ya kwenda na kurudi, gharama za chakula na huduma nyingine ikiwemo ya
wakalimani,’’ alisema Bw Patrick Magai, Meneja Maendeleo Viwanda kutoka TCCIA.
Wakizungumza
wakati wa kongamano hilo lililofutiwa na Uzinduzi wa Klabu wa Wafanyabiashara
ya Benki hiyo mkoani humo, baadhi ya washiriki walisema pamoja na huduma za
kifedha ipo haja ya taasisi za kifedha hapa nchini kuongeza ushirikiano zaidi
na wafanyabiashara hao pindi wanapotafuta zabuni kubwa zenye kuhitaji dhamana
kutoka taasisi hizo.
“Pia
ipo haja kwa taasisi za fedha nchini kutambua baadhi ya changamoto
zinazotukabili wateja wao kwenye biashara zetu kwa kubuni huduma zinazotambua
changamoto zetu ikiwemo kuangalia namna ya kushirikiana nasi pindi tunapokabiliwa
na changamoto ya ucheleweshwaji wa malipo yetu kutoka kwa wateja wetu,’’
alisema mmoja wa wafanyabiashara hao ambae ni Mkandarasi, Dr Steven Masangia.
No comments:
Post a Comment