November 25, 2019

SHULE ZA MJI WA NZEGA ZATAKIWA KUWA NA MASHAMBA DARASA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Nzega Philemon Magessa (kulia) akitoa ufafanuzi jana wakati wa kikao cha robo ya kwanza cha Baraza la Madiwani.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Nzega William Jomanga (katikati) akisitiza jambo wakati akifungua jana kikao cha robo ya kwanza cha Baraza la Madiwani. (Picha na Tiganya Vincent).

Na Tiganya Vincent

MADIWANI wa Halmashauri ya Mji wa Nzega wameshauriwa kuhakikisha kila Shule katika Kata zao inakuwa na mashamba darasa kwa ajili ya uzalishaji wa mazao mbalimbali ikiwemo ya chakula.

Hatua itaziwezesha Shule kuwa na chakula ambacho kitatumiwa na wanafunzi na hivyo kuongeza usikivu wawapo kwenye masomo.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo William Jomanga wakati akifungua kikao cha robo ya kwanza ya Baraza la Madiwani.

Alisema pamoja na kuwasahauri wazazi wajenge desturi ya kuchangia chakula kwa ajili ya watoto wao mashuleni ili kuongeza kiwango cha ufaulu pia ni kila shule iwe na shamba la mfano kwa ajili ya uzalishaji wa chakula cha wenyewe.

Jomanga alisema kuwa zipo shule zina mashamba ni vema wakatumia maeneo hayo kulima mashamba ya mfano ambayo yatawapa chakula na wananchi watakwenda pale kujifunza.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mteandaji wa Halmashauri ya Nze Mji Philemon Magesa alisema ufaulu wa wanafunzi unategemea ushirikiano baina ya wazazi , walimu na jamii ikiwemo kuhakikisha watoto wanapata chakula cha mchana.

Alisema wakitambua kuwa watoto wanahitaji chakula cha mchana shule watachangia kwa kuzingatia utaratibu ambao watakubaliana na kuwaweza watoto wao kupata mlo wa mchana na hivyo kuwaongezea utulivu.

No comments:

Post a Comment

Pages