November 20, 2019

TANESCO WATAKIWA KUMALIZA MIRADI KWA WAKATI

Hafsa Omar - Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewaagiza mameneja wa wilaya za Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kusimamia na kuhakikisha miradi yote ya umeme ya mkoa wa Dar es Saalam inakamilika kwa wakati.

Ametoa agizo hilo, Novemba 18, 2019 wakati alipokuwa na ziara ya kukagua maeneo ambayo bado hayajapatiwa umeme na kukagua uboreshaji wa miundombinu ya umeme na kuwasha umeme katika kata ya msumi, wilaya ya Ubungo mkoa wa Dar es Saalam.

Aidha, amewataka mameneja hao kuhakikisha miradi yote ya umeme inamalizika kwa haraka ili waanza kuandaa miradi mengine ambayo wananchi wa jiji la Dar es Salaam wanaisubiria kwa muda mrefu.

“kitendo cha kuweka nguzo na nyaya halafu kazi haiendelei kinawakatisha wananchi tamaa ya kupata umeme, ni bora tujielekeze kwenye mradi mmoja unakamilika halafu unaenda kwenye mradi mwengine kwa upande wangu miradi ikisimama miaka miwili naita ni matumizi mabaya ya fedha”.

Pia amewaomba wananchi wa Dar es Saalam kutoa taarifa kuhusu miradi ambayo imekaa kwa zaidi ya miaka miwili ambayo bado haijaendelezwa kwani kucheleweshwa kwa miradi hiyo ni upotevu wa fedha za walipa kodi.

Alisema, Serikali inawahidi kazi ya usambazaji umeme nchi nzima na itaendelea kufanya hivyo hata kwenye maeneo ya majiji makubwa.

Aidha, alisema katika kuona umuhimu wa kusambazaji wa umeme katika maeneo hayo Waziri wa Nishati wakati anazindua bodi ya wakurugenzi ya Tanesco,amewaelekeza wajumbe hao kutembelea maeneo haya ili kuhakikisha umeme unafika kila mahali katika nchi yetu.

Vile vile, amewataka Tanesco inafute njia ambayo itawaezesha wananchi kulipia umeme kidogo kidogo haswa wale wananchi wenye kipato cha chini ili nao wanaidike na nishati hiyo ya umeme.

Naye Bi Josephine Mtani ambae ni mkaazi wa mtaa wa kibesa amsema amefurahishwa kwa kitendo cha Serikali kuanza peleke umeme kwenye maeneo yao, kwani walikuwa wanasubiri umeme kwa mda mrefu.

“ Tulikuwa tumesahaulika lakin tunaishukuru Serikali hii kwa kutukumbuka kwakweli wananchi wa kibesa tumefurahi sana kwa ujio huu wa umeme” .

Katika ziara hiyo Naibu waziri aliambana na Mkuu wa wilaya ya Ubungo Mh kisare Makori, mbunge wa jimbo la Kibamba John Mnyika, alitembele maeneo mbali mbali ya Mpigi magoi,Kibesa na Msumi.

No comments:

Post a Comment

Pages