November 13, 2019

TMDA YABAINI AINA SABA YA DAWA FEKI

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA), Akida Khea akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) mapema wakati wa kutangaza matokeo ya ukaguzi maalum wa dawa  vifaa tiba, vitendanishi, dawa asili na tiba mbadala, tukio lililofanyika makao makuu ya TMDA, Mabibo Jijini Dar e Salaam.


Na Asha Mwakyonde

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), imebaini aina saba za dawa bandia katika ukaguzi maaluma wa dawa, vifaa tiba, vitendanishi na dawa asili za tiba mbadala ambazo zinathamani ya Sh. Milioni 12. 5.

Ukaguzi huo maalumu ulifanyika kwa kushirikiana na ofisi ya Rais, Baraza la Famasia, Baraza la Dawa Asili na Tiba Mbadala na ofisi ya Rais (Tamisemi) Oktoba 8 hadi 11 mwaka huu katika maeneo 558 kwenye  wilaya 33 za Mikoa 20.

Akizungumza na waandishi wa habari keo Novemba 13 , 2019 jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Akida Khea alisema dawa zilizokamatwa ni Sonader Cream 10gm, Gentrisone Cream 10gm, Sulphadoxine Pyrimethamine, Alprim, Homidium Chloride, Cold cap na Temeva NDV strain.

“Hizi dawa tumebaini ni bandia baada ya operation maalum iliyofanyika kuna Sodium cream toleo namba A1912 na A1758 ni bandia, Gentrison cream toleo namba GNTRO X031  na tarehe ya kutengenezwa 21/04/2019 ni bandia.

“Kuna za kopo  =ambazo ni Sulphadoxine Primethamine hii kopo la dawa husika lina namba ya kughushi ya usajili namba TAN 05.412.102.FAST kuna Alprim toleo namba 6L74 na tarehe ya kutengenezwa ya Oktoba 2018 ni bandia.

“Homidium Chloride makopo matatu ya dawa hii ya mifugo inaonekana kutengenzwa  na ki9wanda cha Ciplaya India ambacho hakitengenezi dawa za mifugo  na makopo mengine suta yanaonesha yametengenezwa  na kiwanda cha Malleus Chem Ltd ya Kenya taarifa ambazo sio ya kweli na ni bandia.

“Zingine ni Cold cap dawa hii inadaiwa kutengenezwa nchini India ambapo jina la kiwanda haipo kwenye kifungashio wakati dawa halisi ni COLDCAP ambayo inatengenezwa na kiwanda cha REGAL Pharmaceuticals Ltd cha Kenya.

“Dawa nyingine ni Temevac NDV strain 1 na 2 dawa hii bandia umeandikwa kwa kiingereza  na inamakosa ya kisarufi katika lebo dawa hizi hasi zinatengenezwa na kiwanda cha serikali cha TVI na imethibitisha kuwa dawa hizi ni bandi,”alisema Khea.

Kwa mujibu wa Khea katika ukaguzi uliofanyika pia dawa ambazo hazijasajiliwa zilikamatwa zenye thamani ya Sh 31,934,360 na dawa za Serikali zenye thamani ya Sh 481,600.

“Dawa hizo ambazo hazijasajiliwa zilikuwa ni kapsuli za dawa inayotambulika kwa jina la Indowin, vidonge vya dawa vyenye mchanganyiko wa Artesunate na Amodiaquine,kapsuli za dawa iliyojulikana kwa jina la Coldwin na dawa ya sindano ya Magnesium Sulphate.

“Dawa za Serikali zilizokamatwa ni chupa za dawa na sindano ya oxytocin, vidoge aina ya Bigomet, vichupa tisa, dawa za vidongo yenye kutibu malaria na zingine pia zilikamatwa katika maduka ya watu binafsi.

“Pia tulikamata vifaa tiba vyenye thamani ya Sh 640,000 kati yake ikiwa ni Sugical blades na H.pylori rapid test na vifaa tiba vya serikali vyenye thamani ya Sh 224,300, operation pia ilibaini vifaa tiba ambavyo havujasajiliwa vyenye thamani ya Sh 16,384,750,”alibainisha Khea.

Alisema kutokana ukaguzi huo mpaka sasa watuhumiwa wameshafikishwa katika vyombo vya usalama ambapo jumla ya majalada 19 ya kesi yameshafunguliwa katika vituo mbalimbali vya polisi.

“Aidha ufuatiliaji  kupitia vyombo vya usalama unaendelea kuwabaini wale wote waliojihusisha na uingizaji ,utengenezaji na usambazaji wa dawa bandia.

Khea alisisitiza kuwa pamoja  akubainika kwa uwepo wa dawa na vifaa bandia lakini zipo dawa halisi na zilizosajiliwa na TMDA zenye majina kama hayo.

Hata hivyo alitoa wito kwa wananchi kuhakiksha wanapata dawa kutoka katika vituo vya kutolea huduma za dawa vunavyotambuliwa na serikali  ikiwa ni pamoja na maduka ya dawa yaliyosajiliwa  na serikali kupitia  taasisi zake na kupewa risiti baada ya kununua.

“Endapo watabaini kuwa matoleo ya dawa zilizobainishwa kuwa ni bandi wanashauriwa kuzirudisha dawa hizo katika ofisi za TMDA au ofisi za serikali zilizo karibu na wao na kwa lengo la kulinda afya ya jamii wananchi wanaombwa kutoa taarifa  kuhusu mtandao wa wale wote wanaojihusisha na usambazaji,utengenezaji, uingizaji na  wiziwa dawa,vitendanishi na vifaa tiba vya bandia au vya serikali.

No comments:

Post a Comment

Pages