November 23, 2019

RAIS MAGUFULI AWASIMAMISHA KAZI VIGOGO POLISI

Ndugu wanahabari;

Napenda kuwafahamisha kwamba Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, amewasimamisha kazi kuanzia leo tarehe 23/11/2019 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP RICHARD GEORGE ABWAO na RCO Mkoa wa Shinyanga SSP JOHN NDIBALEMA RWAMULEMA ili kupisha uchunguzi.

Sababu za kusimamishwa kwao kazi ni kutokana na kushirikiana na Wamiliki wa kiwanda cha kutengeneza pombe kali cha CANON cha mkoani Shinyanga kukwepa kulipa kodi.

Sababu ya Pili ni Utovu wa Nidhamu kwa kushindwa kutekeleza maelekezo waliyopewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo Mhe, Zainab Telack.

Imetolewa na:
David A. Misime - SACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma, Tanzania

No comments:

Post a Comment

Pages