November 23, 2019

WAZAZI WAIOMBA SERIKALI KUPUNGUZA GHARAMA ZA MATIBABU YA WATOTO NJITI

Daktari Bigwa wa Watoto Wachanga kutoka Hospitali ya Aga Khan, Dk. Yaser Abdallah, akizungimza na waandishi wa habari.

Na Asha Mwakyonde

NCHINI Tanzania watoto 255,000 huzaliwa  wakiwa njiti kati ya watoto milioni 1.5 wanaozaliwa kila mwaka huku kiwango cha vifo vya watoto hao kufikia asilimia 21  kwa vizazi hai 1000.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es SalaamNovemba 22, 2019  katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto Njiti Dunia  Mkuu wa Idara ya Watoto kutoka Hospitali ya Aga Khan, Dk. Mariamu Buran, amesema idadi kubwa ya watoto hao wanaofanikiwa kuishi wanaendelea kuwa na hatari  ya muda mrefu.

Dk. Mariamu amefafanua hatari hiyo ikiwa ni pamoja na kupata matatizo ya kujifunza,ukiziwi  na upofu  ambspo ni miongoni mwa mengine mengi.

Dk. Mariamu amesem kuwa matatizo ya uzazi njiti yanachangia kwa asilimia 30 ya vifo vinavyotokea mwezi wa kwanza tangu mtoto kuzaliwa.

Amesema watoto  takribani milioni 15 huzaliwa njiti duniani kote  sawa na mtoto mmoja katika kila vizazi 10 na asilimia 60 ya watoto hao wanazaliwa Afrika na Asia kusini.


Kwa upande wake Dk. Bingwa wa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati Dk. Yaser Abdallah, amesema  watoto 20 hufariki dunia kila mwaka kutokana na matatizo yanayosababishwa na uzazi njiti..

Baadhi ya wazazi ambao walizaa watoto kabla ya wakati  Beatrice Mbawala  na Sudi Abubakari  wameiomba serikali na wadau mbalimbali kuangalia namna ya kupunguza gharama za matibabu na kuweza kuwaongezea muda wa likizo ya uzazi kutokana na watoto hao kuhitaji uangalizi wa hali ya juu..

Maadhimisho ya Uzazi njiti Dunia hufanywa kila mwaka November 17 ambapo mwaka huu kaulimbiu yake ni "kutoa tiba sahihi, kwa wakati mwafaka na mahali sahihi".

No comments:

Post a Comment

Pages