December 10, 2019

AFRIKA NI BARA LA NURU- BABA WA UZAO

Baba wa Uzao wa Kanisa Halisi la MUNGU BABA akiwahutubia waumini wa Kanisa hilo (hawapo pichani) hivi karibuni.
 
Waumini wa Kanisa Halisi la MUNGUN BABA wakiwa katika moja ya Ibada za Kanisa hilo.
Na Mwandishi Wetu, Arusha
KANISA  Halisi la MUNGU BABA limesema Afrika ni Bara lenye nuru kubwa na si  sehemu yenye giza kama linavyosemwa.
Kauli hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa miaka mingi ya waafrika kuaminishwa kuwa Bara lao ni sehemu ya giza na hakuna nuru yoyote inayopatikana ili hali inarasilimali za kutosha ikiwemo madini,mito,mabwawa,bahari,misitu wakiwemo viumbe mbalimbali wa baharini na wanyamapori.
Akizungumza na mamia ya  wananchi na waumini wa Kanisa hilo katika Mji Mdogo wa Namanga wilayani Longido Mkoa wa Arusha, Baba wa Uzao wa Kanisa hilo amesema Afrika ni Bara la nuru  na si la giza
Amesema kwa kuwa utendaji wa nafsi ambao ulikuwa unaruhusu watu kuibiana vipawa, karama,talanta na viwekezo sasa umefika kwenye ukomo.
Amesema hicho ndicho kilikuwa kilele cha ubaya wa kila aina kwa kuonea na kumzonga mwingine na hatimaye kumwangamiza kwa sababu tu ya vitu vizuri alivyopewa na MUNGU BABA.
Amesema kwa Tanzania heri  imeanza kuonekana kwa maana ya kuishi unachosema, kuishi ya moyoni siyo ya mdomoni na Moyo wako kusomeka usoni kwako.
“Wengi hawajajua kwa nini Rais Dk. John Magufuli  amefanikiwa ndani ya muda mfupi na kwa nini anapendwa na MUNGU BABA, ni kwa kuwa anaishi kile anachosema na huko ndiko kuishi Moyo”amesema Baba wa Uzao
Amefafanua kuwa sauti mpya iliyoanzia Tanzania, Afrika, kwenda katika Mataifa mengine, ndicho kitu kikubwa ambacho kinasababisha sasa Afrika iwe nuru siyo giza kama linavyosemwa.
Amesema matatizo yote ya Afrika, asilaumiwe yeyote, bali kulikiuwa na vitu vitatu ikiwemo Vita na Ufunuo ambayo ilikuwa inawaingia wale wote ambao wanaonekana  ni wakorofi.
“Giza, kwa maana ya umasikini na ubaya tunaoona katika Bara la Afrika, narudia kusema kuwa, ilikuwa ni hii miduara mitatu.
“Hata yule mwandishi wa Kitabu Kikubwa, aliyekiweka kwenye google, kuwa Afrika ni Bara la giza, aliingiwa na ufunuo,nyoka na vita, maana hizo ndizo nafsi zilizokuwa zinajua kuwa Afrika ni nuru, wakageuza kibao kuwa ni giza”amesema Baba wa Uzao

No comments:

Post a Comment

Pages