December 03, 2019

AJINYONGA KWA KATANI HADI KUFA

Na Lydia Lugakila, Kagera

 Mtu mmoja mkazi wa Kijiji cha Rushwa Kata ya Mshabago wilayani Muleba mkoani Kagera amekutwa amejinyonga kwa kamba ya katani na kupoteza maisha.

Mtendaji wa kata hiyo, Goreth Gervaz,  amemtaja aliyejinyonga kuwa ni Frank Angero mwenye umri wa miaka 29 mkazi wa kitongoji cha Buyango  ambapo taarifa za tukio hilo zimebainika Decemba 3 mwaka huu kijijini hapo.

Gervaz amesema kuwa marehemu amekutwa amejinyonga nyumbani kwake kwa kutumia kamba na hakuacha kujumbe wowote unaoelezea chanzo cha yeye kufanya hivyo.

‘’Kwenye nyumba yake mwenyewe majirani walisema walifika wakapiga hodi bila kumuona mhusika baada ya kusogeza pazia wakaona amening’inia na kuwa chanzo cha tukio hilo bado kinachunguzwa alisema mtendaji  huyo.

Ameongeza kuwa kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita marehemu na mke wako walikuwa na migogoro ya kifamilia iliyosababisha wanamfuata mtendaji huyo hadi maeneo yake ya kazi.

Kwa upande wake shemeji wa marehemu Edwin kazimili amesema kuwa baada ya kupata taarifa alienda nyumbani kwa marehemu na kukuta amejinyonga.

Naye mke wa marehemu Jastina Frank amesemakuwa tukio hilo lilitokea wakati akiwa hayupo nyumbani kwani alikuwa amekwenda kwa wazazi wake kwa ajili ya kumuona mtoto aliyekuwa anaumwa.

No comments:

Post a Comment

Pages