Na Mwandishi Wetu
BENKI ya NMB imetwaa tuzo maalum kutoka Bodi ya Taifa ya Uhasibu
na Ukaguzi wa Hesabu(NBAA) kama Benki bora ya Taarifa za Kifedha
zilizokaguliwa na kutambuliwa kimataifa kwa mwaka 2018,ilikoshinda benki
kadhaa nchini.
Benki hiyo imetambuliwa kwa kufikia kiwango bora katika
utayarishaji wa taarifa zake za kifedha, kulingana na mahitaji ya
taarifa (viwango vya kuripoti za kitaifa na kimataifa).
Hafla ya kukabidhiwa tuzo hiyo ambayo kwa NMB, ni ushindi wa mara
ya pili mfululizo, ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
ambapo NBAA ilisema taarifa za mahesabu za NMB zimeendelea kuwa bora
kila mwaka, ubora uliowasukuma majaji kuwapa tuzo
hiyo kwa mara nyingine.
Akizungumzia vigezo vilivyotumika kupata washindi, Mkurugenzi
Mtendaji wa NBAA Mr.Pius Maneno, amesema walipatikana kwa kuangalia
washiriki waliovuka asilimia 75 ya vigezo vilivyowekwa.
Naye Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Mr. Benedicto Baragomwa,
amesema wao kama wataalam wa masuala ya fedha, wanatambua umuhimu wa
kuandaa vitabu vya mahesabu vya Benki kwa njia na mifumo inayozingatia
viwango vya kitaifa na kimataifa.
“Ushindi huu unadhihirisha namna ambavyo tumejikita katika
kudumisha uadilifu wa hali ya juu kwenye uwasilishaji wa taarifa zetu za
kifedha za mwaka,” alisema Baragomwa baada ya kupokea tuzo kutoka kwa
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Amina
Shabani.
Baragomwa alibainisha kuwa, wawezeshaji wa benki hiyo wameandaliwa
katika misingi inayofuata na kuheshimu viwango vya kimataifa
vinavyotambuliwa na IFRS, pamoja na mahitaji ya ndani.
Taarifa iliyotolewa na Benki hiyo imetoa shukrani kwa wafanyakazi
na kujivunia mfumo bora wa Uongozi na utendaji hasa kitengo cha fedha.
"Tuzo hii imepatikana nyuma ya mfumo uliopo wa utawala bora na michakato
ya udhibiti ambayo inakuza uwazi wa taarifa
za kifedha, uwajibikaji,ueledi na kiwango cha juu cha uadilifu wa
takwimu. Hongera kwa kila mtu, haswa timu ya kifedha kwa kuongoza
maandalizi ya Taarifa ya Fedha ya Benki ya NMB.
#NMBKaribuYako
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamis Shaabani,
akimkabidhi Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa,
Tuzo ya Benki Bora katika utayarishaji wa
ripoti za kifedha kwa mwaka 2019, iliyotolewa na Bodi ya Taifa ya
Ukaguzi wa Hesabu (NBAA). Hafla ya kukabidhiwa tuzo ilifanyika jijini
Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. (Na Mpiga Picha Wetu).
Kaimu
Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa, akionesha Tuzo
aliyoipokea ya Benki ya NMB kuwa Benki Bora katika utayarishaji wa
ripoti za kifedha kwa mwaka 2018, iliyotolewa
na Bodi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu (NBAA).
Kaimu
Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa (wa pili kulia)
akiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake wakati wa utoaji tuzo.
No comments:
Post a Comment