December 07, 2019

Chuo Kikuu Mzumbe chaongeza wanafunzi, kozi

Na Irene Mark

UONGOZI wa Chuo Kikuu Mzumbe, umejivunia kuongeza idadi ya wanafunzi kutoka 166 hadi 1,033 na kozi kufikia 10 kutoka mbili za awali kwenye kampasi yake ya Da es Salaam.

Licha ya mafanikio hayo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Lugano Kusiluka, alisema wahitimu wa chuo hicho wameandaliwa kukabiliana na ushindani kwenye soko la ajira kwa kujiajiri na kuajiriwa kwa tija.

Akizungumza jijini Da es Salaam jana wakati wa mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Kusiluka alisema ubora wa kitaaluma unaopatikana chuoni hapo umeongeza chachu ya wahitimu bora wanaoweza kukabiliana na changamoto kwemye jamii.

"Napenda kuwahakikishia wote mliojiunga nasi Ieo katika mahafali haya kuwa, tumewatayarisha wahitimu hawa kukabiliana na changamoto mbalimbali katika sehemu zao za kazi kwa kutumia elimu, ujuzi na maarifa waliyopata hapa chuoni na kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa azma ya Serikali ya viwanda kuelekea uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

"...Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2005 Chuo cha Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam kimeendelea kukua kwa kuongeza idadi ya wanachuo na programu za masomo, hiyo ni ishara kwamba tunafanya kitu bora," alisema Profesa Kusikila.

Kwa mujibu wa Profesa Kusiluka kampasi hiyo kwa sasa ina wanafunzi 416 wanao endelea na masomo darajani na wengine 617 wanaofanya tafiti katika maeneo mbalimbali ili kukamilisha tasnifu zao.

Alisema Kampasi inaendesha madarasa ya kujiandaa kwa ajili ya mitihani ya ngazi ya juu ya uhasibu, yaani, 'Certified Public Accountant (CPA)' inayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Tanzania (NBAA).

"Kutokana na ubora wa mafunzo yanayotolewa na wataalamu wetu, kwa miaka minne mfululizo madarasa haya yamekuwa yakifanya vizuri sana kwa mujibu wa taarifa za NBAA.

".,,Katika mahafaIi ya 41 ya NBAA ya mwaka 2019, Kituo cha Chuo cha Kampasi ya Dar es Salaam cha Kikuu Mzumbe kilizawadiwa cheti cha ufaulu bora zaidi yaani kati ya vituo vyote vinavyoendesha mafunzo hayo. Tunawakaribisha wote wenye nia ya kujiaanda kwa ajli ya mitihani ya NBAA kujiunga na madarasa hayo hapa chuoni," alisema Profesa Kusiluka.Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, CPA. Pius Maneno, alisema uongozi wa baraz hilo unakabiliana na changamoto ya wahitimu kukosa ajira ambayo kwa sasa wanakabiliana nayo kwa mbinu tofauti.

Aliitaja moja ya mbinu hizo kuwa ni kuanzisha kambi ya ujasiriamali inayofanyika kila mwaka huku akiwaasa wahitimu waliomaliza Chuo Kikuu Mzumbe kuhakikisha wanatumia akili, maarifa na elimu waliyoipata chuoni hapo kutatua changamoto na kuziona fursa kwenye jamii zao.

Mlau Cyriacus Binamungu akiongoza maandamano ya mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam yaliyofanyika leo Desemba 6, 2019. Jumla ya wahitimu 445 wametunukiwa shahada zao huku wanawake wakiwa 236 na wanaume 209.

Brass Band ikiongoza maandamano.

Maandamano kuelekea ukumbini.


Baadhi ya wahitimu.

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Jaji Mstaafu, Barnabas Samatta, akitangaza kuanza rasmi Mahafali ya 18 ya chuo hicho Kampasi ya Dar es Salaam.







Muhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Dk. Seif Muba, akiongoza shughuli za mahafali.
 

Mlau Cyriacus Binamungu akitoa hotuba yake wakati wa Mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam yaliyofanyika Desemba 6, 2019.

Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, CPA. Pius Maneno akitoa hotuba yake.

Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, CPA. Pius Maneno akitoa hotuba yake.

Wahitimu wakiwa katika mafahali.

Mkamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka akitoa hotuba yake.

Mkamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka akitoa hotuba yake.

Muhitimu akisikiliza kwa makini hotuba ya Makamu Mkuu wa Chuo.


Wahitimu.

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Prof. Honest Ngowi, akitangaza kuwatambua wanachuo na wanataaluma waliofanya vizuri.

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Jaji Mstaafu Barnabas Samatta, akimkabidhi cheti mmoja wa wanafunzi waliofanya vizuri.

No comments:

Post a Comment

Pages