December 18, 2019

CHUO KIKUU MZUMBE KAMPASI YA DAR CHATOA SEMINA KUHUSU NAMNA YA KUBORESHA TAALUMA YA UGAVI NA USAFIRISHAJI

Na Boniface Mande

Chuo Kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na shirika la usafirishaji na ugavi KUEHNE ya nchini Uswisi wameendelea kutoa mafunzo ya namna ya kuboresha shughuli za ugavi na usafirishaji nchini kupitia semina zinazofanyika chuoni hapo.
 
Akizungumza na mwandishi wetu Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe Dkt. Omary Swalehe, amesema kuwa mafunzo hayo ni ya nne kufanyika chuoni hapo chini ya msaada wa Shirika la KUEHNE kama sehemu ya kutoa msaada wa kitaalamu kwa wanafunzi wa mafunzo ya ugavi na usafirishaji pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya ugavi na usafirishaji.
 
Ameongeza kuwa semina hiyo ya siku tatu ilikuwa na lengo la kutoa msaada wa kitaaluma kwa wanafunzi pamoja na wadau wa sekta ya ugavi na usafirishaji nchini katika kuboresha shughuli za ugavi na usafirishaji ili kuleta tija na kuongeza mapato katika sekta husika.
Bosco Mapunda akitoa mada kwenye semina ya namna ya uendeshaji wa shughuli za ugavi na usafirishaji iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam. Semina hiyo imefadhiliwa na shirika la KUEHNE kama sehemu ya kutoa msaada wa kielimu katika sekta ya ugavi nchini.
Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt Omary Swalehe, akichangia mada  katika semina ya namna ya uendeshaji wa shughuli za ugavi na usafirishaji iliyofanyika katika Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam. 
Magoma Aloyce kutoka Kampuni ya Hillbrokes akichangia mada katika semina ya namna ya uendeshaji wa shughuli za ugavi iliyofanyika Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam. Semina hii imefadhiliwa na shirika la KUEHNE kama sehemu ya kutoa msaada wa kielimu katika sekta ya ugavi nchini.
Mmoja wa washiriki, Birungo Ngero Lyasi, kutoka Chuo Kikuu Mzumbe akichangia mada kwenye semina ya namna ya uendeshaji wa shughuli za ugavi na usafirishaji uliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam. Semina hii imefadhiliwa na shirika la KUEHNE kama sehemu ya kutoa msaada wa kielimu katika sekta ya ugavi nchini. 
Dkt. Maige Mwasimba, kutoka Chuo Kikuu Mzumbe akichangia mada wakati wa semina ya ya namna ya uendeshaji wa shughuli za ugavi na usafirishaji iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam. Semina hiyo imefadhiliwa na shirika la KUEHNE kama sehemu ya kutoa msaada wa kielimu katika sekta ya ugavi nchini.
  Baadhi ya washiriki wakisikiliza kwa makini somo kwenye semina ya namna ya uendeshaji wa shughuli za ugavi na usafirishaji iliyofanyika Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam.
Florence Singano kutoka TASAC akichangia mada wakati wa semina ya ya namna ya uendeshaji wa shughuli za ugavi na usafirishaji iliyofanyika Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Pages