Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya CRDB, Stephen Adili,
akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo
vikuu ijulikanayo kama 'Boom Advance' uliofanyika wakati wa tamasha la
michezo la CRDB TOT Bonanza wikiendi hii.
Mkuu wa
Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya CRDB, Stephen Adili (katikati) akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi na wafanyakazi wa benki
hiyo wakati wa uzinduzi wa huduma ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu
ijulikanayo kama 'Boom Advance' uliofanyika wakati wa tamasha la michezo
la CRDB TOT Bonanza wikiendi hii.
Na Mwandishi Wetu
Benki ya CRDB imezindua mikopo
maalum kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo vikuu ijulikanayo kama “Boom Advance”,
uzinduzi huo umefanyika katika tamasha la michezo la ‘CRDB Bank – TOT Bonanza’
na kuhudhuriwa na wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali katika mkoa wa Dar es
Salaam.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi wa Benki ya CRDB, Stephen Adili alisema huduma
ya Boom Advance imelenga katika kuwasiaidia wanafunzi kutatua changamoto ya
kifedha pindi wawapo vyuoni.
“Kwa muda mrefu tumekuwa tukiangalia ni kwa namna gani tunaweza kuipatia
suluhisho changamoto hii ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa inachangia kuathiri
masomo ya wanafunzi,” alisema Adili.
Adili alisema mkopo huo wa Boom Advance unatolewa kidijitali kupitia
huduma yetu ya SimBanking App, ambapo ni njia rahisi itakayowawezesha wanafunzi kufurahia huduma
hiyo wakiwa chuoni bila kutembelea benki jambo ambalo lingeweza kuingiliana na
muda wa masomo.
“Tumefanya hivi tukifahamu kuwa wanafunzi wengi wa vyuo wapo
katika kizazi cha kidijitali,” aliongezea Adili.
Ili kupata huduma ya Boom Adavance mwananfunzi anatakiwa kuwa mnufaika
wa mkopo kutoka Bodi ya Mikopo HESLB na kusajiliwa katika mfumo wa Benki wa
utoaji mikopo kidijitali “Digital Disbursment System”.
Akiongelea baadhi ya sifa na faida za Boom Advance Adili alisema mkopo
huo wa Boom Advance unamuwezesha mwanafunzi anaweza kukopa kuanzia TZS 40,000
hadi TZS 120,000 bila riba huku muda wa kurejesha mkopo ukiwa hadi siku 45
tokea kuchukua mkopo, ambapo alisema muda huo umezingatia mpaka mwanafunzi
atakapo pata mkopo mwengine kutoka HELSB.
Adili alisema katika mkopo huo wa Boom Advance malipo yanafanyika moja
kwa moja baada ya mkopo kuingia kwenye akaunti ya mwananfunzi, lakini pia mwanafunzi
anaweza kufanya malipo (yote/sehemu) mwenyewe bila kusubiri hela ya mkopo
kutoka HELSB kuingia.
Alizungumza kwaniaba ya wanafunzi wa vyuo vikuu mwanafunzi wa Chuo cha
Kodi, Catherine Constatine ameishukuru Benki ya CRDB kwa kuanzisha huduma hiyo
ya Boom Advance huku akisema itakwenda kuwa mkombozi kwa wanafunzi wengi
hususan katika kipindi ambacho wanakuwa wakisubiri mkopo kutoka HELLSB au pindi
wanapoishiwa fedha.
Hivi karibuni Benki ya CRDB pia ilifanya maboresho katika Akaunti ya ya
wanafunzi ya scholar ambapo hivi sasa akaunti hiyo haina makato ya aina yoyote,
mwanafunzi pia anaunganishwa na mifumo ya kidijitali itakayomuwezesha kupata
huduma za benki popote pale alipo ikiwamo TemboCard, SimBanking, Internet
banking na CRDB Wakala
Tamasha hilo pia liliambatana na michezo mbalimbali ambapo timu za mpira
wa miguu na kikapu za Benki ya CRDB na timu za vyuo vikuu ziliumana vikali.
No comments:
Post a Comment