Mfungaji wa bao pekee la timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ Ditram Nchimbi (kulia), pamoja na kiungo wa timu hiyo, Hassan Dilunga wakishangilia bao hilo katika mchezo dhidi ya Zanzibar katika michuano ya CECAFA inayoendelea nchini Uganda. (Picha na TFF).
Na John Marwa
Timu ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' imezindukia kwa ndugu zao wa Damu Zanzibar Heroes kwa kuwaweka bao 1-0, mchezo wa pili Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na kati CECAFA.
Kilimanjaro wamepata ushindi huo kwa kazi nzuri iliyomaliziwa na Ditram Nchimbi kwenye mchezo wa kuvuja jasho na Damu.
Kwa matokeo hayo Kilimanjaro Stars wamefikisha pointi 3 baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Mashemeji zao Kenya mchezo wa ufunguzi.
Mchezo unaofuata Kilimanjaro Stars watashuka dimbani kesho kutwa kumenyana na Sudan.
Mchezo wa awali Sudan walimenyana na Kenya mchezo uliomalizika kwa Kenya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Kwa ushindi huo Kenya wametinga hatua ya nusu fainali wakishinda mechi mbili dhidi Kilimanjaro na Sudan .
Kilimanjaro wnashika nafasi ya pili wakiwa na pointi tatu za mechi mbili huku Zanzibar wakikalia nafasi ya tatu na pointi moja sawa na Sudan wanaobuluza mkia kwa tofauti ya mabao ya katika msimamo wa kundi B.
Kilimanjaro watakwaana na Sudan wakihitaji pointi tatu kusonga mbele huku Kenya wakipapatuana dhdi ya Zanzibar ambao watakuwa wanausaka ushindi huku wakiwaombea njaa Kilimanjaro.
Mchezo wa Zanzibar dhidi ya Kenya utakuwa wa marejeano ya fainali ya msimu uliopita ambapo Kenya waliibuka mabingwa kwa mikwaju ya penati.

No comments:
Post a Comment