Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amesema kuwa katika kuhakikisha
tunakuza uchumi wa Viwanda, Wilaya hiyo imeandaa maonesho ya wajasiriamali wa bidhaa zangozi yatakayofanyika Disemba 12
hadi 15 katika viwanja vya Tanganyika Packers.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo, Mhe. Chongolo amesema kuwa maonesho hayo ambayo
yata ambatana na uuzwaji wa bidhaa hizo yatafanyika ikiwa ni katika mkakati wa
kutangaza na kuhamasisha wananchi kutumia bidhaa zinazo zalishwa hapa nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo. |
Amesema kuwa
lengo la maonesho hayo ni kutangaza uwezo wa wadau wa ngozi, kuelimisha jamii
kujenga utamaduni wa kutumia bidhaa hizo zenye ubora zinazozalishwa hapa nchini
sambamba na kuongeza soko la ajira kwa vijana.
Amefafanua
kuwa katika maonesho hayo yatahusisha wajasiriamali kutoka Wilaya ya Kinondoni
pamoja na Halmashauri nyingine zilizo alikwa ikiwemo Ilala, Temeke, Ubungo
pamoja na Kigamboni.
Mhe.
Chongolo amefafanua kuwa kupitia sensa ya mwaka 2012, Manispaa ya Kinondoni
inajumla ya wakazi zaid ya milioni 1.3, ambapo idadi hiyo inategemea kupata
bidhaa za ngozi, ikiwemo Viatu, Mikanda, Mabegi na pochi zinazo tokana na
bidhaa za ngozi.
Mhe.
Chongolo ameeleza kuwa hali hiyo imekuwa tofauti kutokana na watu hao kutumia
bidhaa zinazozalishwa kutoka nje ya nchi na hivyo kuwasihi wannachi kupenda
kutumia bidhaa zinazo zalishwa hapa nchini.
“Tanzania
ni miongoni mwa nchi kubwa barani
Afrika zinazo zalisha ngozi kwa kiasi kikubwa , lakini pia Tanzania ni
miongoni
mwa nchi tatu Afrika zenye mifugo mingi
, Tanzania ni Nchi pia ambazo
zinatumia bidhaa hizo kwa wingi, mfano rekodi inaonyesha kuwa jumla ya
viatu zaidi ya milioni 53 zinaingia na kutumika kila mwaka” ameeleza
Mhe. Chongolo.
Rais wetu
mpendwa, Dk. John Magufuli kila siku amekuwa akisisitiza kujenga viwanda ili
kufikia uchumi wa kati, na sisi wasaidizi wake tunaliangalia hilo kwa kulifanyia
kazi, ndio mana tumeona tuwaweke pamoja wajasiriamali wa bidhaa za ngozi, na
hatutaishia hapa tunampango mwakani tuyafikishe mbali zaidi” amesema Mhe.
Chongolo.
Serikali ya
Viwanda, Mhe. Chongolo amefafanua kuwa pamoja na kwamba Tanzania inazalisha ngozi
nyingi lakini ipo changamoto kubwa inayotokana na malighafi hizo kusafirishwa
nje ya nchi jambo ambalo amesema limesababisha kuwepo kwa uhaba wa ngozi kwa
ajili ya uzalishaji wa bidhaa hizo.
Hata hivyo
Mhe. Chongolo amesema kuwa kauli mbiu ya maonesho hayo ni Kinondoni yetu,
Viwanda vyetu, Tanzania yetu ambapo kupitia maonesho hayo itakuwa ni fursa kwa
vijana wengi kujiajiri , kuongeza pamoja na kukuza viwanda vya ndani vya ngozi
na hivyo kuongeza uzalishaji na ubora wa bidhaa hizo.
No comments:
Post a Comment