December 30, 2019

MAKOSA DHIDI YA BINADAMU YAONGEZEKA MKOANI KAGERA

Kamanda wa Polisi Mkoani wa Kagera, Revocatus Malimi.


Na Lydia Lugakila, Kagera

Jeshi la Polisi mkoani Kagera limepunguza makosa ya maadili makosa ya mali na makosa dhidi ya binadamu kutoka makosa 3201 mwaka 2018 kufikia makosa 2749 2019.


Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi, amesema kuwa pamoja na jeshi kufanya jitihada hizo bado makosa dhidi ya binadamu yakiwemo ya ubakaji, mahuaji na ulawiti yameongezeka kutoka makosa 427 mwaka 2018 kufikia makosa 432 mwaka 2019.


Kamanda Malimi amesema makosa ya mahuaji watu kujiua yameongezeka kutoka mahuaji 158 mwaka 2018 hadi makosa hadi makosa 163 kufikia Desemba 22 mwaka huu.


Wakati huo huo Amesema makosa ya ubakaji yameongezeka kutoka makosa 243 mwaka kufikia makosa 244 huku makosa ya unyanga’nyi wa kutumia siraha na upatikanaji wa noti bandia yakiwa yamepungua kutoka makosa 1438 hadi makosa 1041.


Ameongeza kuwa mbali na jitihada hizo bado makosa ya ajali za barabarani yameongezeka kutoka ajali 24 zilizosababisha vifo 40 mwaka 2018 kufikia ajali 38 zilizosababisha vifo 41 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Pages