Na Janeth Jovin
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, kutumikia kifungo cha miaka miwili jela au faini ya Sh.500,000 baada ya kutiwa hatiani katika shtaka moja la kutengeneza nyaraka za uongo kati ya 30 aliyokuwa akikabiliwa nayo.
Mbali na Malinzi, mwingine aliyehukumiwa ni aliyekuwa katibu wa shirikisho hilo, Slestine Mwesigwa, ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka minne jela au kulipa faini ya Sh. Milioni moja baada ya kutiwa hatiani katika mashtaka mawili.
Aidha mahakama hiyo imewaachia huru washtakiwa wawili katika kesi hiyo ambao ni aliyekuwa mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga na Karani wa TFF, Frola Rauya ambaye kutokana na upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao.
Hukumu ya Malinzi na wenzake ambao wamesota mahabudu kwa miaka miwili na nusu imechukua takribani saa 5 ambapo ilianza kusomwa saa 8:30 mchana hadi saa 12 jioni.
Hata hivyo mahakama hiyo ilikwama kusoma hukumu hiyo zaidi ya mara tatu mfululizo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo Hakimu aliyetakiwa kusoma hukumu hiyo kutokuwepo kutokana na kuhamishwa kituo cha kazi.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi, Maira Kasonde, alisema amepitia ushahidi wa pande zote mbili baina ya utetezi na mashitaka ambapo amewatia hatiani washitakiwa katika makosa mawili kati ya 30 yaliyokuwa yakiwakabili.
"Kwa maana hiyo Mahakama inaona mshitakiwa wa kwanza na wa pili wana hatia kwa shitaka la pili na mshitakiwa wa pili ana hatia katika shitaka la nne,"alisema Hakimu Kasonde.
Akitoa adhabu Hakimu Kasonde alisema shtaka la pili ambalo ni kughushi nyaraka kila mshtakiwa atakiwa kulipa faini ya Sh.500,000 ama kifungo cha miaka miwili jela na kwa mshtakiwa wa pili katika kosa la nne la kuwasilisha nyaraka za uongo Benki anatakiwa kulipa faini ya Sh.500,000 ama kwenda jela miaka miwili.
Pia Hakimu Kasonde alisema mahakama hiyo imewakuta washtakiwa hao hawana hatia katika mashtaka 18 ikiwemo la utakatishaji fedha.
Aidha alisema washtakiwa wote walikuwa wanakabiliwa na mashtaka 30 na baadae mahakama iliwaona hawana kesi ya kujibu katika mashtaka 10 ambayo ni ya matumizi mabaya ya ofisi, kughushi nyaraka, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji fedha.
Alisema katika mashtaka ya kujipatia fedha ambayo yalimkabili Malinzi, upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha mashtaka hayo kwa sababu fedha alizozipata Malinzi kutoka TFF ni aliikopesha shirikisho hilo kama inavyothibitishwa na maofisa wanne waliotoa ushahidi mahakamani hapo.
Pia alisema upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashitaka hayo kwa kutoleta ripoti ya ukaguzi ya kuonesha fedha zilizopokelewa ni halali au la.
Katika mashtaka ya utakatishaji fedha yaliyowakabili Malinzi, Mwesigwa na Nsiande, Hakimu Kasonde alisema mashtaka hayo hayajathibitishwa kwa sababu fedha anazodaiwa kupokea Malinzi ambazo ni Dola za Marekani 173,335 na Sh 39,100,000 ni marejesho ya mkopo aliokopesha TFF.
"Ni maoni yangu kwamba shtaka la utakatishaji fedha lilipaswa kueleza ni matendo gani aliyafanya mshtakiwa ambayo yalisababisha utakatishaji," alisema Hakimu Kasonde.
Awali kabla ya hukumu hiyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon aliiomba mahakama itoe adhabu kali Kwa washtakiwa hao ili iwe fundisho kwa wengine.
Naye Wakili wa utetezi, Nehemia Nkoko alidai kuwa washtakiwa hao ni makosa yao ya kwanza kutenda na hawajawahi kushitakiwa.
"Pia mshitakiwa Malinzi anawatoto na amekamatwa akiwa na miaka 58 na sasa ana miaka 60, pia ana matatizo ya Kiafya,"
Kuhusu mshtakiwa wa pili, Wakili Nkoko amedai kuwa ana Mama wa miaka 89 anaumwa, pia ana mtoto wa miaka 4 na wakati anakamatwa alikuwa na miaka 47 hivyo na yeye anaelekea kwenye uzee.
"Tunaomba iwapatie unafuu wa adhabu,"alisema.
Awali kesi hiyo ilikuwa na mashtaka 30 lakini ilipofikia katika uamuzi wa kama washtakiwa wana kesi ya kujibu ama la walipunguziwa mashtaka 10 na kubakiwa na mashitaka 20.
Upande wa Jamhuri katika kesi hiyo ulikuwa na mashahidi 15 na vielelezo tisa.
Katika hatua hiyo mshtakiwa watano Miriam Zayumba aliachiwa huru kwa sababu alionekana hana kesi ya kujibu kwa mashtaka yote yaliyokuwa yakimkabili.
Kwa pamoja walikuwa wanakabiliwa na mashtaka 20 katika kesi ya jinai namba 213 ya mwaka 2017.
Miongoni mwa mashitaka yao ni kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa Dola za Marekani 173,335.

Aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
Jamal Malinzi (katikati) akiwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wake, Selestine
Mwesigwa pamoja na Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga, wakiwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo wakati wa
kusomewa hukumu yao. (Na Mpiga Picha Wetu).
Aliyekuwa Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga (kulia) akikumbatiwa na mama yake mdogo baada ya kuachiwa huru katika ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi akiwapungia mkono ndugu na jamaa waliofika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo baada ya mahakama hiyo kuwahukumu kulipa faini ya jumla ya Sh. Milioni 1.5 au kwenda jela miaka minne kwa makosa mawili, Jamal Malinzi na Selestine Mwesigwa. Kosa la kwanza washtakiwa wote faini ya 500,000 kila mmoja au kwenda jela.

No comments:
Post a Comment