Nyumba za walimu zilizojengwa katika Chuo cha Ualimu Mpuguso na kukamilika kwa ubora.
Moja ya bweni lililojengwa kwa ubora katika Chuo cha ualimu Mpuguso mkoani Mbeya.
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Elimu, Sayansi Na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amemuagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Leonard Akwilapo, kusimama kwa karibu ujenzi wa miundombinu ya Chuo cha Ualimu Mpuguso, Mkoani Mbeya.
Ujenzi wa miundombinu hiyo unatekelezwa na Mkandarasi Lukolo Construction Company na kuhakikisha ukamilishaji wa kazi hiyo unafanyika kwa wakati ili majengo hayo yaweze kutumiwa na walimu tarajali.
Waziri Ndalichako ameagiza hayo leo Desemba2,2019 baada ya kukagua mradi huo na kukuta ukitekelezwa kwa hali isiyoridhisha na katika baadhi ya maeneo kuwa chini ya kiwango.
Alisema mkandarasi huyo pamoja na kushindwa kukamilisha kazi yake kwa wakati aliepewa muda zaidi ili kukamilisha kazi hiyo lakini ameshindwa na kusababisha chuo kushindwa kutumia miundombinu hiyo na Serikali kuchelewa kufikia malengo yake ya uboreshaji na upanuzi wa chuo hicho.
"Naelekeza mradi huu ukamilike ifikapo Desemba 30 tena kwa ubora kama ilivyopangwa hivyo Katibu Mkuu afuatilie kwa karibu kazi hii na makandarasi akishindwa kukamilisha mchukulie hatua," amesema Ndalichako
Kiongozi huyo alisema kwa mujibu wa makubaliano mapya baada ya kurudishwa kazini ni kukamilisha kazi hiyo lakini hata sasa haonekani kuwepo eneo la mradi na hakuna kinachoendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, amemweleza waziri kuwa mkandarasi huyo asipokamilisha kazi hiyo kwa muda uliopangwa atachukuliwa hatua na kuwa kama mkoa watafuatilia pia utekelezaji wake kwa karibu.
Katika hatua nyingine Chalamila amemwomba waziri wa elimu kukipatia chuo hicho gari ili kusaidia katika huduma mbalimbali jambo ambalo Waziri aliridhia na kusema kuwa tayari wizara imenunua magari kwa ajili ya vyuo vya ualimu ambavyo havina huduma hiyo.
Mkuu wa Chuo cha Ualimu Mpuguso, Dorothy Mhaiki ameishukuru Serikali kwa namna inavyoboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia katika chuo hicho na kuomba kukarabati maeneo mengine yaliyobakia kwa kuwa bado kuna uhitaji ikiwemo kusaidia kupatikana watumishi walinzi na wapishi ili kupunguza gharama ya uendeshaji.
Ukamilishaji wa ujenzi wa miundombinu katika Chuo cha Ualimu Mpuguso ni sehemu ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa ujenzi na ukarabati wa miundo mbinu katika Chuo hicho ambao umegharimu kiasi cha sh bilioni 10 unaotekelezwa na serikali ya Tanzania na ile ya Canada.
Mradi huo umetekelezwa na kandarasi mbili Salem Construction Ltd ambao wamekalilisha kazi zao kwa ubora na majengo kuanza kutumika na Lukolo Construction Company ambao bado kazi yao haijakamilika.

No comments:
Post a Comment