December 02, 2019

MRADI WA KUIMARISHA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA PWANI NA BAHARI WAZINDULIWA DAR


Na Asha Mwakyonde


NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, amesema kuwa sekta ya uvuvi inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo miundombinu hafifu ya kuhifadhi samaki inayochangi ubotevu mkubwa (Post -harvest loss), baada ya mavuno hususani kipindi cha mvua.

Haya ameyasema jijini Dar es Salaam leo Desemba 2, 2019 wakati akizindua mradi wa kuimarisha usimamizi wa rasilimali za Pwani na bahari kwa kiwango cha kimataifa unaojulikana kama  Binadamu na Uhifadhi Hai ( Man and Biosphere Reserve), katika Wilaya tatu za Kibiti Mafia na Kilwa.

Amesema kuwa changamoto nyingine ni ukosefu wa mitaji kwa wavuvi na soko la uhakika wa mazao ya uvuvi, uwekezaji mdogo kwenye sekta hiyo hususan katika uvuvi wa barari kuu na uuzaji wa viumbe maji pamoja na kuendelea kuwapo kwa uvuvi haramu.

" katika kukabiliana na changamoto hizi moja ya mikakati ya Wizara ni kuimarisha ushirikiano na taasisi zisizo za kiserikali na taasisi za kiraia kuhakikisha rasilimali za uvuvi zinasimamiwa, kuendelezwa kwa njia endelevu," amesema Ulega.

Amesema moja ya taasisi muhimu ni Shirika la World Wide Fund for Nature  (WWF), ofisi ya Tanzania kupitia miradi mbalimbali iliyotekelezwa na shirika hilo katika eneo la uvuvi.

Naibu Waziri huyo ameeleza kuwa wizara inatambua  na kuthamini mchango mkubwa wa WWF Tanzania katika kulinda rasilimali za uvuvi za a uvuvi kuanzia miaka ya 1990 hadi sasa.

 Amesema mafanikio yaliyopatikana kupitia miradi iliyotekelezwa na WWF ni kuanzisha eneo la usimamizi la RUMAKI linalojumuisha  Halmashauri za Rufiji, Mafia na Kilwa na kwamba eneo hilo limekuwa la mfano kwa miradi mingi ya maendeleo..


Kwaupande wake Muhifadhi Mkuu wa WWF, Dk. Simon Lugandu amsema mradi uliozinduliwa ni mwendelezo wa kazi ambazo WWF imekuwa ikiwekeza katika eneo la mradi kwa miaka zaidi ya 15 katika Pwani ya Bahari ya Hindi.

Amsema  mradi umelenga kuimarisha usimamizi na utunzaji wa rasilimali za pwani ya bahari katika wilaya za Kibiti, Mafia na Kilwa pia kuimarisha usimamizi wa rasilimali katika eneo la Tengefu la Bahari katika kisiwa cha Mafia.

"Pamoja na eneo la uwanda wa bahari wa RUMAKI kutambuliwa kimataifa kama RAMSAR site mradi huu unakusudia kuinua eneo hilo kuwa kiwango cha kimataifa katika kundi la Binadamu na hifadhi"amesema.

Muhifadhi huyo ameeleza kuwa  katika Ukanda wa bahari ya WWF imekuwa ikishirikiana na serikali, idara na wizara husika kwa kipindi kirefu kuanzia miaka 1990 kunusuru rasilimali za bahari na pwani ili ziweze kuwa na manufaa kwa wanajamii na uchumi wa Taifa.

"Jitihada zilianza katika wilaya ya Mafia na baadaye kupanuka kwenda Kibiti na Kilwa, WWF iliendelea kuweka mikakati zaidi na mwaka 2013 kazi za mradi zilipanuliwa kwenda katika Wilaya ya Kigamboni na Mtwara Vijiji"ameeleza..

Amefafanua kuwa  programu hiyo imewekeza katika ushirikishaji wa jamii katika kusimamia rasilimali za pwani na bahari kwa kuwawezesha uanzishaji wa vikundi vya usimamizi shirikishi, kutoa mafunzo na kuwajengea uwezo wanajamii kuhusu usimamizi na matumizi endelevu ya rasilimali.

Naye Mratibu wa mradi, Modester Medard amesema mradi huo umegharimu sh bilioni 10.1 na utatekelezwa kwa muda wa miaka mitano ambapo utakamilika Julai 2024.

" Mradi huku hautatoa ufadhili kwa marine park mpya narudia tena mradi huu hautatoa ufadhili kwa marine park park mpya,"amesisitiza Modester.

Amesema kuwa mradi huo ni wa kuendeleza ushiriki wa jamii katika kuondoa umasikini,kuimarisha vikundi vya maendekeo.

No comments:

Post a Comment

Pages