December 27, 2019

MSITUMIE VIBAYA MADARAKA-TUGHE

Na Asha Mwakyonde

BAADHI ya Wakuu wa majengo (Block Managers), wakuu wa Idara  na wakuu wa vitengo wamekuwa wakiwanyanyasa watumishi walio chini yao kwa kutumia vibaya  mamlaka  waliyopewa.

Haya ymesemwa leo Disemba 27, 2019 na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa serikali na sekta ya afya  (TUGHE), tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Mziwanda Chimwege, wakati akisoma risala fupi ya
mkutano mkuu wa mwaka kwa mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Mhimbili Prof. Lawrence Museru.

Amesema changamoto  kuna baadhi ya wakuu wa idara wamekuwa wakitumia madaraka yao vibaya kwa kuwanyanyasa watumisi waliochini yao.

Amesema changamoto nyingine ni wakuu wa idara kutotambua umuhimu wa chama cha wafnyakazi mahali pa kazi  na kusababisha hamasa ndogo  ya wafanyakazi hao kujiunga na TUGHE.

“TUGHE tunaona hili si sawa na si dalili njema katika kujenga taasisi yetu ili iweze kufikia matumini na mtarajiao ya Watanzania waliowengi, wanotarajia kupata huduma  bora na za uhakika kutoka kwetu.Tunaomba hatua za haraka zichukuliwe ili kuthibiti hali hii,”amesema Chimwege.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa ulipaji wa posho (Allowances), mbalimbali bado haujawa umzuri kutokana na kutolipwa  kwa wakati mfano malipo ya bima  pamoja na malipo y likizo.

Aidha mwenyekiti Chimwege amesema kuwa tawi hilo linawanchama 908 na kwamba wanashirikiana vizuri katika kutatua changamoto zilizopo na kuweza hali ya utulivu na amani ndani ya tsisi hiyo.

Chimwege ameushukuru uongozi wa hospitali ya Muhimbili kwa kushirikiana na tawi hilo katika masula mbalimbali yakiwamo ya vikao vinavyohusu maboresho ya posho.
Akifungua mkutano huo Prof. Museru amesema kuwa  uongozi wa hospitali hiyo utaendelea kushirikian na taasisi hiyo kwa lengo la kuleta tija katika masula mbalimbali  yenye maslahi kwa wafanyakazi wake.

“Uongozi wa hoapitali ya Muhimbili haupo tayari kuona wakuu wa idara wakiwanyanyasa waliochini yao, hatua kali zitachukuliwa dhidi yao. Pia hospitali imejitahidi  kutokuweka malimbikizo kwa wafnyakazi wake, hata hivyo kuna chngamoto ya rasilimali fedha kwani hazipo za kutosha,”amesema Prof. Museru.

Aidha Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa watafuatilia changamoto zinazojitokeza kwa  wanachama hao wa TUGHE tawi la Muhimbili  hasa kwa wasataafu kwa lengo la kupatiwa stahiki zao kwa wakati.

Akimshukuru Mkurugenzi huyo, Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam, Tabu Mambo, amesema  wanajivunia kuwa na tawi la Muhimbili  ambalo ni miongoni mwa tawi kubwa Tanzania nzima huku likiongoza kuwa na wanachama wengi na kwa upande wa kipato pia linaongoza.

“Tawi hili pia linaongoza kwa kuwapatia mafunzo viongozi waajiri wa wamatawi Tanzania nzima na hii inonyesha ile sheria ya mahusinamo kazini unaitekeleza vizuri,”amesema Tabu Pia amemshukuru Mkurugenzi huyo Prof.Museru kwa kufadhili shughuli zinazofanya n TUGHE tawa la Muhimbili kwa kughramia gharama mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Pages