Mkuu wa Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, Deodatus Kinawilo, akiwaongoza kukagua ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Bukoba.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Dkt. Bashiru Ali, akizungumza wakati wa ukaguzi wa hospitali ya wilaya ya Bukoba.
Na Lydia
Lugakila, Kagera
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Dkt. Bashiru Ali, ameagiza viongozi wa Serikali
za vijiji kuacha mara moja ugawaji na uuzaji wa
ardhi za vijiji kwa watu binafsi wenye uchu wa madaraka,
wanaojilimbikiza mali badala yake ardhi
hiyo itumike kwa matumizi ya maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.
Dkt. Bashiru ametoa kauli hiyo akiwa
katika Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera katika ukaguzi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo
iliyopo eneo la Bujuna ngoma.
Aidha Dkt. Bashiru akikagua mradi wa ujenzi wa Hospitali ya wilaya hiyo
ametoa pongezi kwa wananchi wa Kijiji
cha Kanazi kwa kutoa ardhi kwa ajili ya
maendeleo na kuagiza viongozi wa Serikali za vijiji kuacha mara moja ugawaji na
uuzaji wa ardhi za vijiji kwa watu
binafsi wenye uchu wa madaraka wanaojilimbikiza mali badala yake itumike kwa matumizi ya Maendeleo ya wananchi
na taifa kwa ujumla.
Katibu huyo amesema kuwa
kwa kipindi cha nyuma tatizo
hilo limekuwepo ambapo wenyeviti, na watendaji wake pamoja na halmashauri ya
kijiji wamekuwa wakigawa ardhi kwa watu
binafsi wenye lengo kujilimbikizia mali
kuliko kuwekeza katika masuala ya maendele.
‘’Natoa maelekezo kwa
wanaogawa ardhi ya kijiji hawana mamlaka hayo ardhi ya kijiji hata kama ni
hatua moja igawiwe kisheria na ni lazima mkutano mkuu wa kijiji uhusishe watu
wenye umri wa miaka 18 wanaoishi eneo husika
wawepo wasajiliwe kwamba wameudhulia na muhtasali uwepo hapo ndo ardhi
ya kijiji itaruhusiwa kugawanywa’’ alisema Katibu huyo.
Amesema Wenyeviti wa vijiji waliochaguliwa hivi karibuni
wanapaswa kusimamia sheria za ardhi na kuwa ardhi inabidi igawiwe na mkutano mkuu wa kijiji na sio
mwenyekiti wa kijiji.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa
hospitali ya wilaya mkurugenzi wa
Halmashauri ya wilaya ya Bukoba Solomon Kimilike amesema mradi huo umeanza januari 26, 2019 na umeghalimu Shilingi
milioni 1.5 huku akitaja mradi huo kukumbwa na changamoto ya baadhi ya mafundi
jamii waliopewa kazi ya ujenzi kuiba baadhi ya vifaa vya ujenzi ikiwemo chokaa
pamoja na Masinki.
Akijibu taarifa hiyo ya Mkurugenzi Dkt Bashiru amewaagiza wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa
nchini kuhakikisha miradi yote
inakotekelezwa hakuna udokozi.
Hata hivyo kwa upande
wake Harouna Rweyongeza Swarehe ambaye ni mwananchi kijijini hapo amewapongeza wananchi
waliojitolea ardhi kwa ajili ya
maendeleo na kuongeza kuwa uwepo wa hospitali hiyo umesaidia pakubwa kwani kwa
muda wamekuwa wakifuata huduma ya
matibabu umbali wa kilometa 20 kutoka maeneo hayo na kuifuata hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kagera kupata matibabu.
No comments:
Post a Comment