December 02, 2019

MTANZANIA VICTOR JOSEPH AIBUKA MSHINDI TANZANIA OPEN 2019

 Mshindi wa Mikwaju ya jumla wa mashindano ya gofu ya Tanzania Open 2019 M Chadha kutoka klabu ya Kili  mara baada ya kupokea zawadi kutoka kwa Mwakilishi kutoka kampuni ya Oryx Energy Sira Muhele katika mashindano yaliyomlizika katika Uwanja wa Kili Jijini  Arusha.
 Mshindi wa jumla wa mashindano ya gofu ya Tanzania Open 2019 Victor Joseph kutoka klabu ya Gymkhana mara baada ya kupokea zawadi kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mh Dumbaro  katika mashindano yaliyomlizika katika Uwanja wa Kili Jijini  Arusha.


SELEMANI SEMUNYU

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa  Mh Damas Ndumbaro amehitimisha  Mashindano ya Gofu ya Wazi ya Tanzania Open jijini Arusha huku mcheza gofu Victor Joseph  kutoka klabu ya Gymkhana ya Dar es Salaam akitwaa ubingwa wa mashindano hayo

Mchezaji huyo kutoka Klabu  ya Dar es Salaam Gymkhana alifanikiwa kubakiza kombe baada ya kuibuka mshindi wa mashindano hayo yaliyoshirikisha wachezaji toka Nchi Sita kwa kupata Mikwaju (Gross) 294.

Siku ya kwanza Mchezaji huyo alicheza 75,74,71 na 74 akifuatiwa  Joseph Chinywai kutoka Uganda aliyepata mikwaju  308 na kuwashinda wachezaji wengine wa  divisheni A walioshiriki mashindano hayo.

Katika  Mikwaju ya jumla Net Manraj Chadha wa kili golf aliibuka na Ushindi baada ya kupata  Mikwaju ya Jumla 291 huku akiwa amecheza 72,74,71 na 74 katika mzunguko wa Mwisho.

Mshindi katika Divisheni B ni  Joe Lee ambaye alipata mikwaju ya jumla 149 baada ya kucheza 71 na 78 katika  mzunguko wa pili huku kiwango chake cha makosa kikiwa ni 18.

Mshindi katika  kundi la senior ni Boniface Nyiti wa Lugalo aliyepiga Mikwaju yaa Jumla 162 baada yaa mzunguko wa kwanza kupata mikwaju 81 sawa na mzunguko wa pili huku kiwango cha makosa kikiwa ni Nane.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Mwenyekiti wa TGU Criss Martin alisema mashindano haya ni mashindano ya 69 tangu kuanzishwa kwake lakini kumekuwa na Changamoto nyingi na kuomba Rais Magufuli kutupia Jicho mchezo huo.

“ tunatambua kazi kubwa ya Mh Rais katika Majukumu mbalimbali ambayo amekuwa akifanya lakini tunaomba atupie jicho pia Mchezo huu umekuwa  na mafanikio” Alisema Mwenyekiti.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ndumbaro aliahidi kufikisha kilio chao kwa wahusika ili kuendeleza mchezo huu nap engine kwa kuanzia ngazi yaa Mashuleni ili kupata vipaji na kuzalisha wachezaji bora wakiwemo wa kulipwa

“ Nitafikisha Kilio chenu Serikali ili kuboresha Mchezo huu lakini pia hakikisheni mnasajili viwanja ili viwango vya Uchezaji viweze kutambulika Kimataifa “. Alisema Naibu Waziri Ndumbalo.

Aidha alisema Mashindano yamefanikiwa  na hiyo ni kutokana na Kazi nzuri waliyofanya kwa kushirikiana na na kamati ,waratibu Verge Africa na wadhamini ambaao wamefanya Zawadi kuwa Bora hivyo inahitaji kuendelezwa.

Klabu za Tanzania zilzoshiriki mashindano haya yaliyodhaminiwa na Oryx, Super Doll, Garda word, Coca Cola, Tanfoam, Hal na Serengeti ni Lugalo, Dar es Salaam Gymkhana zote za Dar es Salaam, Morogoro Gymkhana, Arusha Gymkhana, TPC, Moshi na Zanzibar Sea Cliff .

No comments:

Post a Comment

Pages