Mkuu
wa Kitengo cha Kadi wa Benki ya NMB- Philbert Casmir, akizungumza
wakati akifunga rasmi mafunzo ya matumizi ya huduma mpya ya
MastaBoda kwa waendesha Bodaboda wa Wilaya ya Kisarawe na vitongoji
vyake. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo na Mkuu wa
Kitengo cha Biashara za Serikali wa NMB-Vicky Bishubo.
Mmoja wa waendesha Bodaboda akifungua akaunti ya NMB.
Waendesha Bodaboda wakifurahia jambo wakati wakiendelea na mafunzo ya matumizi ya huduma mpya ya MastaBoda.
Waendesha Bodaboda katika picha ya pamoja baada ya semina iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za Wilaya ya Kisarawe.
Na Mwandishi Wetu
KAMPENI ya MastaBoda inayoendeshwa na Benki ya NMB kwa ajili ya kuwaunganisha waendesha Bodaboda katika mfumo wa kibenki wa kupokea malipo kwa Mastercard QR kutoka kwa wateja wa Benki ya NMB, Benki zilizounganishwa na Mastacard QR pamoja na mitandao ya simu iliyounganishwa na huduma ya Mastercard QR sasa imevuka boda hadi Kisarawe Mkoani Pwani.

Akizindua kampeni hiyo na
kufunga mafunzo ya siku sita yaliyotolewa na NMB kwa waendesha Bodaboda
Wilayani humo, Mkuu wa Wilaya Jokate Mwegelo amesema kampeni hiyo imefika muda
muafaka katika Wilaya yake.
Jokate amesema, kama Wilaya na
Serikali wamejipanga kuipokea kampeni hiyo kwa waendesha bodaboda 150 waliyozitokeza
katika mafunzo hayo.
Amesema kupitia kampeni hiyo
wanataka vijana wawe mstari wa mbele katika kujenga uchumi wa nchi na maendeleo
ya jamii zao. Pia amewataka vijana kuishi kwa malengo kwani sasa wamepata
mfumo ambao unaipa ulinzi fedha wanayoipata katika kazi zao za kila siku.
Aidha Jokate ameimwagia kongole
Benki ya NMB kwa kuipa heshima Kisarawe kuwa sehemu ya pili kufikiwa na
MastaBoda baada ya kuzinduliwa Dar es Salaam miezi miwili iliyopita.
"Nashukuru sana NMB kwa
kunipa heshima hii kwa Wilaya yangu ya Kisarawe, naamini hamkupanga kuanzia
hapa baaada ya Dar es Salaam, ila mmeona jitihada zangu asanteni
sana. Hakuna mafanikio bila nidhamu, NMB mmetuletea nidhamu ya pesa pamoja
na usalama kwa vijana wetu maana sasa hawatakuwa wanatembea na pesa
mfukoni."amesema Jokate.
Nae Mkuu wa Kitengo cha Biashara
za Serikali wa NMB, Vicky Bishubo amesema NMB imejipanga kuyafikia makundi
mbalimbali ya wajasiriamali ili kuwaongeze thamani katika kukuza uchumi wa
nchi.
Amesema MastaBoda ni kampeni
ambayo inalengo la kuwafikia waendesha bodaboda zaidi ya Milioni 2 nchi nzima,
ila kufikia 2020 watakuwa wamewafikia elfu 75.
#NMB Karibu Yako.
No comments:
Post a Comment