Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi,
Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akisistiza kwa
menejimenti ya NSSF, umuhimu wa miradi ya nyumba za NSSF zilizopo katika wilaya
ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam wakati
wa ziara yake ya kukagua uboreshaji wa
miundombinu wa nyumba hizo leo tarehe
18, Desemba, 2019.
Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi,
Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama ameridhishwa na utekelezaji
wa maagizo ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassimu Majaliwa aliyoyatoa mwishoni mwa mwezi
Novemba, mwaka huu baada ya kukagua
miradi ya nyumba za NSSF zilizopo katika wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Akiongea
mara baada
ya kukagua miradi ya nyumba za NSSF leo Desemba 18, 2019 baada ya
kukagua miradi ya nyumba za NSSF zilizopo wilayani Kigamboni, Jijini Dar
es salaam, Mhe. Mhagama
amesema kuwa Mhe. Waziri Mkuu alielekeza menejimenti ya NSSF Kuharakisha
kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo ili ziweze kutumiwa na watanzania.
Waziri Mkuu
alielekeza menejimenti ya NSSF kuwasiliana na vyuo vikuu na Taasisi za elimu ya
juu na elimu ya kati, Taasisi za Umma ili kuangalia uwezekano wa wanafunzi
wa elimu ya juu na watumishi wa umma pamoja
na watanzania wenye nia ya kutaka kupanga nyumba hizo waweze waweze kupangishwa
kwenye nyumba za hizo 161 zilizoko Tuangoma, 720 zilizoko
Mtoni Kijichi.
“Nimefurahishwa katika taarifa yenu kuwa
mmewasiliana na vyuo kadhaa ikiwemo DUCE ambao wameonesha nia ya kuomba nafasi
za wanafunzi 3000, lakini pia DIT wanahitaji nafasi za wanafunzi 300,
tunawasubiri IFM na taasisi nyingine za elimu ya juu na Umma,kwa kuwa kwa Mradi
wa Kijichi unazo nyumba 720 ambazo zinaweza kupangishwa na wananfunzi 7,200 kwa
mantiki hii inaonesha tunao uwezo wa kukidhi mahitaji ya vyuo vikuu ”
Amesema Mhe.Mhagama.
Mhe. Mhagama, ameongeza
kuwa katika kuhakikisha nyumba hizo zinakuwa mkombozi wa malazi kwa wanafunzi
wa vyuo, hivyo ameishauri menejimenti ya NSSF kuwapa kipaumbele wanafunzi wa
kike kwa kuzingatia kuwa takwimu za hivi karibuni zimebainisha kuwa maabukizi
mapya ya virusi vya UKIMWI asilimia 40 ni kwenda kwa vijana ambapo asilimia 80
ya vijana ni watoto wa kike wa vyuo vikuu, amabapo mojawapo ya kichocheo cha
maabukizi hayo ni kutokana na kutokuwa
na malazi salama.
Waziri Mkuu,
alielekeza TARURA kuhakiksha wannatengeneza miundombinu ya barabara katika miradi ya
nyumba za NSSF, ambapo tayari wamekamilisha taratibu za awali za ujenzi wa barabara hizo na wataalamu
wa NSSF tayari wamehakiki gharama za ujenzi wa barabara hizo ili kuona kama
zinaendana na uhalisia wa ujenzi utakaofanyika kupitia SUMA JKT. Zahanati
“Katika kuboresha
barabara za mitaa za hizi nyumba nimeonakazi inayoendelea na wameniambia DIT wanafanya kazi yao ya
kuweka taa za sola kwenye barabara za mitaa yote ya
nyumba hizi na watafanya kazi kwa wakati kama tulivyokubaliana” amesema Mhagama.
Aidha, agizo jingine
kwa menejimenti ya NSSF ilikuwa ni kuboresha miundo mbinu ya Umeme, maji taka
na maji safi, ambapo tayari taasisi zinazohusika na miundo mbinu hiyo ikiwemo
TANESCO na DAWASA wamekamilisha taratibu za awali za utekelezaji na wameahidi
kukamilisha shughuli zake kwa wakati ili nyumba ziweze kutumika.
Waziri Mhagama amefafanua kuwa agizo lingine
ambalo NSSF wamelitekeleza ni Mthamini
Mkuu wa Serikali kutathimini nyumba hizo na kutoa bei halisi
ya soko kwa sasa ili kuwawezesha Watanzania wengi na hasa watumishi wa Umma
kununua na kupanga katika nyumba hizo.
“Nimefurahishwa na taarifa mliyonipatia
kuwa mthamini mkuu wa serikali atakabidhi ripoti yake leo kwa NSSF na naamini
sasa watu wengi ambao wameonesha nia ya kupanga au kununua tutawapatia huduma
kwa kuwa tunalo kundi la wanafunzi, watumishi wa umma na watu binafsi wenye
uwezo wa kununua nyumba hizo”, Amesisitiza Mhagama.
Pia, Waziri Mkuu aliagiza Halmashauri ya wilaya ya Kigamboni kupewa
kipaumbele kwa nyumba 439 za Nungu ambapo Mkuu wa wilaya na viongozi
wa Halmashauri ya wilaya ya Kigamboni walielekezwa kuwasaidia watumishi wa
wilaya na Halmashauri hiyo kuingia mikataba rafiki itakayowawezesha
watumishi hao kupewa kipaumbele katika kununua au kupanga kwenye
nyumba hizo mara ukarabati utakapo kamilika.
“Nimeridhishwa na utekelezaji wa shughuli
za miundo mbinu kwa hapa Nungu na hivyo menejimenti ya NSSF wasilianane na Halmashauri
ya wilaya ya Kigamboni kuwa uboreshaji wa majengo unaenda vizuri ili watumishi
tunaowalenga waweze kutumia nyumba hizo, ” Amesema Mhagama.
Pia Mheshimiwa Mhagama amefurahishwa na hatua ya LATRA kuanza kutekeleza agizo la kuanzisha
njia za mabasi ya daladala kupitia kwenye nyumba za NSSF Mtoni
Kijichi na Dungu ili kuwezesha wapangaji na wananchi watakaonunua na kupanga nyumba hizo kupata usafiri wa umma, kama
ilivyokuwa imeelekezwa na Mhe. Waziri Mkuu.
Aidha, Mhe. Waziri pamoja na kuwapongeza
NSSF kuanza kutekeleza maagizo hayo, pia amewataka wazingatie muda uliowekwa wa
kukamilisha kazi hiyo, hivyo amewataka kufanya kazi usiku na mchana kwa
kuzingatia ubora wa kazi.
“Zingatieni uhalisia wa gharama zinazotumika
katika ujenzi wa mradi huu ili fedha za wanachama zitumike vyema kwa kuonekana
fedha zimewekezwa kwenye miradi yenye tija ” Amesema Mhe. mhagama.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, William Erio, amesema NSSF imeyapokea
maelekezo yote yaliyotolewa na Mhe. Waziri Mhagama na kwamba watafanya kwa weledi na ubora ili
kuhakikisha kwamba majengo yote yanakamilika haraka na kuuzwa au kupangishwa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya
Wadhamini NSSF, Balozi Ali Idd Siwa amemhakikishia Mhe. Waziri Kuwa watatoa
ushirikiano wa kutosha katika kuhakikisha kuwa maagizo aliyoyatoa yanatekelezwa
kwa wakati ili kuhakikisha nyumba hizo zinawanufaisha watanzania.
Miradi
ya nyumba za NSSF, wilayani Kigamboni Jijini Dar es salaam, ipo katika maeneo
ya Tuangoma jumla ya nyumba 161,
Dungu nyumba 439 na Mtoni Kijichi jumla ya nyumba 720.
No comments:
Post a Comment