Naibu Waziri wa
Viwanda na Biashara, Mhandisi Stellah Manyanya (wa pili kushoto),
akitoa maelekezo kwa Msajili wa Bodi ya Usajili Wataalamu wa Miapango Miji
nchini, Hellen Mtutwa (kulia), wakati alipotembelea mabanda ya maonesho katika Mkutano
wa Wataalamu wa Mipango mwishoni mwa wiki jijini Dodoma. (Picha na Wizara ya Ardhi).
Naibu Waziri wa
Viwanda na Biashara Eng. Stellah Manyanya
(katikati
waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wataalamu wa
Mipango Miji na baadhi ya wajumbe kwenye Mkutano wa Wataalamu
wa Mipango Miji Nchini uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma.
Na Munir Shemweta, WANMM DODODMA
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
Mhandisi Stellah Manyanya ametaka kushirikishwa kwa sekta ya ardhi hasa idara
ya Mipango Miji katika miradi mbalimbali inayoibuniwa na serikali ili
kuondokana na miradi isiyokuwa na tija kwa jamii.
Mhandisi Stellah Manyanya aliyasema
hayo mwishoni mwa wiki wakati wa mkutano mkuu wa sita wa Mwaka wa Wataalaamu wa
Mipangomiji uliofanyika jijini Dodoma.
Alisema, kumekuwepo na miradi mingi
nchini inayoanzishwa na Serikali na kutumia gharama kubwa lakini matokeo yake imekuwa haitumiki ipasavyo na
wakati mwingine inaingiliana na shughuli nyingine za kijamii hali inayosababisha
kuzuka kwa migogoro kwenye jamii.
Alitolea mfano Jengo la Machinga
Complex lililopo Ilala Jijini Dar es
Salaam, Mhandisi Manyanya alisema, kutokuwepo kwa mipango kina ya muda mrefu na
utafiti duni ndio chanzo kikubwa hadi leo jengo hilo limeshindwa kufikia lengo
walilojiwekea la kuwasaidia wafanyabiashara wadogowadogo katika shughuli zao.
“
Kuna wale wenzetu waliojenga lile
Jengo kubwa kabisa wakalipa jina la heshema Machinga Complex lakini kwa
namna walivyopanga na kutumia fedha kwenye kujenga limebaki kuwa jengo
la aibu” Alisema Mhandisi Stellah Manyanya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi
hiyo Profesa Wilbert Kombe alisema, Miradi Mingi nchini inafanyika bila kushirikisha
wataalamu wa Mipangomiji kwani Taasisi nyingi za Serikali zinapopanga mipango
yake ya kiuchumi na miundombinu hazizingatii na kuonesha mipango ya ardhi
hali inayosababisha muingiliano wa shughuli za kiuchumi.
Aliongeza kwa kusema kuwa, Taasisi
zote nchini zinategemea uwepo wa ardhi, hivyo hazina budi kushirikiana na Sekta
zote zinazohusu ardhi kabla ya kupanga mipango yao ya kiuchumi ili kuepusha
muingiliano na kupangwa vibaya kwa miji.
‘’Ukitazama eneo la Maegesho ya magari ya Mwendokasi eneo la Jangwani Jijini Dar es Salaam , hayo ni matokeo ya
kutoshirikishana katika mipango miji kwani lilile eneo linahitaji mambo mawili
ama lihamishwe au iinuliwe barabara kuanzia Magomeni “ Alisema Profesa Kombe.
Naye Msajili wa Bodi ya Wataalamu
wa Mipango Miji Hellen Mtutwa alisema, taasisi zote za Serikali ni lazima ziwe
na ushirikiano wa karibu wakati wa kuandaa mipango na kuitekeleza siyo sekta za ardhi tu bali Tanesco ,Tanroad
Maji na taasisi nyingine ili kuepusha hasara kwa Serikali .
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa City
Plan Consultants (T) Limited Dkt Juma Mohamed alisema, maendeleo yote yapo
kwenye sekta ya ardhi hivyo Serikali inatakiwa iipe kipaumbele sekta hiyo kwani
hasara ya kutokufanya mipango ni kubwa
kuliko kuitekeleza.
No comments:
Post a Comment