HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 14, 2019

TOC yasaka Mil 97 maandalizi
Olimpiki 2020



Na Mwandishi Wetu, Morogoro


KAMATI ya Olimpiki Tanzania (TOC) inasaka kiasi cha Sh Milioni 97 kwa ajili ya Maandalizi
ya mwisho ya timu ya Tanzania itakayoshiriki Michezo ya 32 ya Olimpiki itakayofanyika
Tokyo, Japan 2020.


Hayo yalielezwa na Mhazini Msaidizi wa TOC, Juma Zaidi wakati wa Mkutano Mkuu uliofanyika mjini hapa katika hoteli ya Kingsway.


Akisoma bajeti hiyo pamoja na zingine Zaidi alisema fedha hizo ni kwa ajili ya maandalizi ya

mwezi mmoja kwa ajili ya timu ya Tanzania itakayoshiriki michezo hiyo.

Zaidi alisema kuwa TOC kwa mwaka 2020 jumla ya bajeti yao ka mwakani ni kiasi cha h
Milioni 640.


“Bajeti ya Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) kwa mwaka 2020 (pamoja na bajeti ya timu ya
Tanzania inayotegemea kushiriki Michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020) ni sawa na fedha za
kitanzania Sh 640,822,723.70.”


Bajeti hiyo ya TOC ya mwaka 2020, pia itahusisha Mkutano Mkuu wa Uchaguzi, ambao
utagharimu kiasi cha Sh Milioni 70 pamoja na Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama cha
Wanaolimpiki (TOA), ambao utatumia kiasi cha Sh Milioni 37.


Alisema kuwa fedha hizo itazipata kutoka katika mapato yatokanayo na Olimpiki Solidarity (OS)
kwa ajili ya mipango ya kipindi chote cha miaka minne (2017-2020), ambacho ni kiasi cha Sh

Milioni 471, hivyo TOC itabidi kusaka kiasi cha Sh Milioni 170 ili kuziba pengo lililopo. Tayari wachezaji wawili wa Tanzania wamefuzo, ambao ni wanariadha Alphonce Simbu na Failuna Abdi kwa ajili ya marathon katika michezo hiyo ya Tokyo itakayofanyika kuanzia Julai 24 hadi Agosti 7, 2020.


Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi akifafanua hilo jana alisema fedha hizo wanatafuta kwa ajili ya kambi ya mwezi mmoja ya maandalizi ya mwisho ya timu hiyo ya Tanzania.

Wiki iliyopita Kamati ya Olimpiki ya Kenya iliidhinisha kiasi cha Bilioni 13 kwa ajili ya ushiriki wa Olimpiki 2020, zikiwemo Bilioni 3 kwaajili ya kufuzu kwa wachezaji kwa michezo hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages