JUMLA ya Sh. Bilioni 216 zimewekezwa katika mfuko wa Umoja (Umoja Fund) na wawekezaji mbalimbali hapa nchini kupitia Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS kuanzia mwezi Mei 2005 mfuko huo ulipozinduliwa hadi Juni mwaka huu.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko wa Umoja (Umoja Fund), Pamela Nchimbi, katika mkutano mkuu wa mwaka uliwashirikisha wawekezaji kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini ili kupata taarifa mbalimbali kuhusu mifuko yote ya UTT AMIS inavyoendeshwa, kupata taarifa za hesabu na kujadili changamoto zilizopo katika uendeshaji na namna ya kuzitatua.
Alisema Mfuko wa Umoja ni mfuko wa kwanza kuanzishwa na UTT AMIS na mpaka sasa mfuko umeendelea kufanya vizuri kwa muda wa miaka 14 mfululizo.
Katika kipindi cha miaka minne mfululizo kuanzia Juni 2015 hadi Juni 2019, ukubwa wa mfuko wa Umoja umekuwa ukipanda na kushuka.
Mnamo Juni 2019, ukubwa wa mfuko wa Umoja uliongezeka kwa shilingi bilioni 4 kutoka shilingi bililioni 212 kama ilivyokuwa juni , 2015 hadi shilingi bilioni 216 mnano juni 2019.
Vile vile thamani ya kipande (NAV) iliongezeka hadi shilingi 576.92 kutoka shilingi 455.50 mnamo Juni 2015 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 27.00.
Akielezea faida ya mfuko alisema faida katika mfuko wa Umoja kwa muda wa miaka minne kwa wastani ilikuwa asilimia 6.44.
Mwaka 2016 faida ilikuwa asilimia 6, mwaka 2017 faida ilikuwa asilimia 6.6, mwaka 2018 faida ilikuwa asilimia 14.45 na mwaka 2019 faida ilishuka mpaka asilimia 1.29.
Mpaka sasa faida jumuishi ya mfuko tangu kuanzishwa ni asilimia 13.42 ingawa kumekuwepo na changamoto kadha wa kadha katika soko la hisa.
Kupanda na kushuka kwa faida na thamani ya kipande cha mfuko wa Umoja imesababishwa na mdororo katika soko la hisa.
“Mwekezaji yeyote anayetaka kuwekeza kupitia mfuko wa Umoja, mfuko wa Umoja unaruhusu mwekezaji wake kuuza vipande vyao wakati wowote hivyo kumpa fursa mwekezaji kupata faida pindi anapozihitaji na kwamba hakuna kiwango cha chini cha uwekezaji kinachoruhusu kupata faida,” anasema.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya UTT AMIS, Casmir Kyuki alisema kuwa ili kuwahudumia wawekezaji kwa njia rahisi zaidi na kupanua wigo kwa wawekezaji, hivi sasa UTT AMIS imezindua mfumo mpya wa tehema unaojulikana kama ‘UTT AMIS APP’ ili kusaidia wawekezaji kununua vipande kwa njia ya simu badala ya kwenda katika ofisi za UTT AMIS kupata huduma.
“Kupitia mfumo huu mwekezaji ataweza kutumia simu kiganjani ( mobile devices ) kupata taarifa za bei ya kipande, kununua kipande kwa simu ya kiganjani, taarifa za uwekezaji, taarifa zote za mifuko ya UTT AMIS, thamani ya kipande cha mfuko wowote na pia kupata taarifa fupi ya akaunti yako (last five transactions) ikiwemo uwekezaji wako,” alisema.
Ili kuweza kupata huduma hii kupitia UTT AMIS APP, mwekezaji lazima ajiunge na huduma ya simu ili aweze kupata huduma hii kwenye kiganja.
Kupitia mfumo huu wawekezaji wanaotumia mtandao wa Tigo-pesa, M-Pesa, Airtel Money, T-Pesa, Halopesa wataweza kununua vipande kupitia simu zao.
“Mwekezaji anaweza kutumia mfumo huu kwa kupiga *150*82# na kasha kufuata maelekezo.” Anasema.
Vile vile maboresho zaidi yanaendelea kufanyika ili kuwawezesha watumiaji wa simu za kisasa (smart phone) kupata huduma kwa urahisi zaidi na kwa kuanzia mifumo ya UTT AMIS imeunganishwa na mifumo ya benki ya CRDB ambayo pia ni msimamizi wa mifuko.
“Hivi sasa mwekezaji anaweza kununua vipande moja kwa moja kwa kutumia mfumo wa benko ya CRDB." Alisema
Pia kwa kuzingatia maendeleo ya soko, wawekezaji wameendelea kupata faida nzuri ikilinganishwa na kigezo linganishi, kigezo linganishi ni wastani wa kipato cha faharisi ya hisa Tanzania kwa asilimia 37.5 na kipato cha dhamana ya serikali ya siku 182 kwa asilimia 62.5 kwa kuzingatia hali ya soko kwa sasa. Mfuko wa umoja ni chaguo zuri la uwekezaji.
Mbali na hilo utendaji wa mfuko katika kipindi cha miaka yote minne (2016,2017,2018 na 2019) umekuwa mzuri.
Faida katika mfuko imekuwa juu ya kigezo linganishi (performance Benchmark) ikiwa ni wastani wa faida ya asilimia kuni (10%) kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Pia katika kipindi hicho chote thamani ya mfuko imeendelea kukua pamoja na idadi ya wawekezaji kuongezeka kutokana na kuongezeka kwa imani na uelewa kuhusu mifuko ya uwekezaji wa pamoja.
Akizungumzia mikakati mingine, alisema kuwa mpaka sasa UTT AMIS imekamilisha utayarishaji wa Mpango Mkakati wa miaka mitano kuanzia (2019/2020 hadi 2023/2024).
Kupitia mpango huu UTT AMIS itaendelea kutoa elimu juu ya faida za uwekezaji ili kufikia wawekezaji wengi, kuboresha huduma kwa wawekezaji na kudhibiti athari katika uwekezaji na masuala mengine.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya UTT AMIS, Casmir Kyuki, akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuanza kwa Mkutano Mkuu wa wawekezaji wa Mfuko wa Umoja uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya UTT AMIS, Issa Wahichenenda, akizungumza katika mkutano Mkuu wa Wawekezaji.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya UTT AMIS, Casmir Kyuki, akizungumza na
waandishi wa habari kabla ya kuanza kwa Mkutano Mkuu wa wawekezaji wa
Mfuko wa Umoja uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya UTT AMIS, Issa Wahichenenda, akizungumza na wawekezaji wa kampuni hiyo katika Mkutano Mkuu wa Wawekezaji uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya UTT AMIS, Casmir Kyuki, akiongoza Mkutano Mkuu wa Wawekezaji wa Mfuko wa Umoja uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Wawekezaji wakiwa katika mkutano huo.
Wawekezaji wakipitia taarifa za mkutano huo.
Mwakilishi kutoka Benki ya CRDB, Mary Mponda, akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya UTT AMIS, Casmir Kyuki, akiongoza Mkutano Mkuu wa Wawekezaji wa Mfuko wa Umoja uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Wawekezaji wakiwa katika mkutano huo.
Wawekezaji wakipitia taarifa za mkutano huo.
Mwakilishi kutoka Benki ya CRDB, Mary Mponda, akizungumza katika mkutano huo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya UTT AMIS, Issa Wahichenenda (kulia), akiteta jambo na Kaimu Mwenyekiti, Francis Chacha.
Mwekezaji akichangia.
Mwekezaji akichangia.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya UTT AMIS, Issa Wahichenenda, akifafanua jambo kuhusu mfuko wa Kujikimu katika Mkutano Mkuu wa Wawekezaji
uliofanyika jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment