Na Sitta Tumma, Mwanza
WATOTO wanaolelewa kwenye Kituo cha NIFO HOPE, jijini Mwanza, wamepewa msaada wa vyakula kwa ajili ya kuimarisha afya zao.
Mbali na chakula, watoto wote wa kituo hicho na wengine zaidi ya 300 wanaolelewa maeneo tofauti, wamepatiwa bima ya afya.
Misaada hiyo imetolewa na Taasisi ya The Desk & Chair Foundation, yenye makazi yake jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation, Alhaj
Sibtain Meghji, ameueleza ulimwengu kuwa watoro wote wana haki sawa,
hivyo matunzo ni lazima.
"Tunazingatia lishe bora, ndiyo maana tumeleta msaada huu
kwa watoto wa kituo hiki kinachoendeshwa a NITETEE FOUNDATION ya Jiji la
Mwanza.
"Ni muhimu sana kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu," amesema Alhaj Meghji.
"Taasisi ya The Desk & Chair Foundation tutaendelea
kuisaidia jamii yenye matatizo, ili kujenga taifa jamii inayopendana,"
amesisitiza Meghji.
Kituo hicho hutoa mahitaji ya maisha kwa watoto, pamoja na TDCF kwa lengo la kuiwezesha jamii kupata faraja.
Watoto hao watapata chakula bora wakati wa kusherehekea
Sikukuu ya Krismasi, inayoadhimishwa ulimwenguni kote Desemba 25 kila
mwaka.
"Tunataka watoto hawa washerehekee na mwaka mpya kwa furaha, kama watoto wengine wote.
"Na watahudhuria shuleni kwa uhakikisho wa milo nzuri
mitatu kwa siku, yaani asubuhi, mchana na usiku," Mwenyekiti wa The Desk
& Chair Foundation, Meghji amesema.
Amewawashukuru wafadhili na watu washirika wengine wenye
mioyo safi, kwa msaada wao wanaoendelea kusaidia watu walio na
upendeleo.
Kwamba misaada hiyo inayotolewa na wafadhili wa The Desk
& Chair Foundation inaunda tumaini la maisha bora kwa jamii yenye
uhitaji.
"Mwenyezi Mungu awalipe wafadhili wetu leo, kesho na hata milele. Aamina," amesema Meghji.
Hata hivyo, uongozi wa Kituo hicho cha NIFO HOPE pamoja na watoto waliopewa msaada huo, wameeleza kufurahishwa na usaidizi huo.
"Tunaushukuru sana uongozi wa The Desk & Chair
Foundation kwa msaada huu. Mungu awabariki daima," amesema mmoja wa
watoto kituoni hapo.
No comments:
Post a Comment