December 21, 2019

WAZIRI KAMWELWE AZINDUA RASMI BARAZA LA 11 LA UONGOZI NIT

 Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi, Profesa Zacharia Mganilwa, akitoa taarifa ya utendaji ya chuo hicho kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, wakati wa uzinduzi wa Baraza la Uongozi la 11 la chuo hicho jijini Dar es Salaam.  

Mkurugenzi wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Kaimu Katibu Mkuu Uchukuzi, CireysonMwaigumbe, akizungumza katika uzinduzi huo.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Uongozi la 11 la chuo hicho jijini Dar es Salaam. 

Mwenyekiti Mpya wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT),  Mhandisi Prof. Bavo Nyichomba akipokea vitendea kazi kutoka kwa  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, mara baada ya kuzindua rasmi baraza hilo leo Desemba 21, 2019. jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti Mpya wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT),  Mhandisi Prof. Bavo Nyichomba, akiangalia kwa makini vitendea kazi alivyokabidhiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwele.
 Mwenyekiti Mpya wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi Prof. Bavo Nyichomba, akitoa hotuba fupi baada ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, kuzindua rasmi baraza hilo leo Desemba 21, 2019. jijini Dar es Salaam.

Picha ya kumbukumbu.

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwele, leo amezindua Baraza la Uongozi la 11 la Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), jijini Dar es Salaam.
Akizindua Baraza hilo Waziri Kamwelwe amewataka wajumbe wa Baraza hilo kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria ili kuisaidia Serikali katika kuhakikisha chuo kinatekeleza vema majukumu yake.
“Chuo hiki ni cha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kinatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria ya Uanzishwaji wake (Na. 24 ya mwaka 1982 (Sura 187 iliyofanyiwa marekebisho 2002) chini ya usimamizi wa Baraza la Uongozi la Chuo kwa niaba ya Serikali. Hivyo mnalo jukumu la kuisaidia Serikali katika kuhakikisha kuwa Chuo kinatekeleza vema majukumu yake.
“Mkasimamie utekelezaji wa mpango Mkakati wa Tatu wa Maendeleo wa Chuo (2015/16 – 2020/2021) ambao unaelekea mwisho.
“Mkasimamie utayarishaji wa Mpango Mkakati wa Chuo wa Nne utakao kidhi mahitaji ya rasilimali watu kwenye sekta ya Uchukuzi na Usafirishaji wakati Serikali ya Awamu ya Tano ikiendelea kujenga Uchumi wa Viwanda katika kulifikisha Taifa kuwa na Uchumi wa Kati ifikapo 2025 kwa kutekeleza miradi mikubwa ya Kimkakati.”amesema Kamwelwe.
Aidha Kamwelwe amelitaka Baraza hilo  kuhakikisha Chuo kinazalisha wataalamu mahiri wenye weledi watakaosimamia uendeshaji wa Makampuni ya Usafiri wa Barabara ikiwa ni pamoja na Kampuni ya Mabasi yaendayo kwa haraka (Bus Rapid Transit - BRT).
Akitoa Tarifa ya Utendaji ya Chuo Mkuu wa Chuo Mhandisi, Profesa Zacharia Mganilwa, amesema Chuo kimejipanga kutekeleza Malengo 11 kwa Mwaka wa Fedha wa 2019/20.
“Lengo la kwanza ni kuongeza mapato ya ndani kutoka Bilioni 14.5 hadi Bilioni 14.8, pili ni kuhuisha mitaaala na kutengeneza mitaala mipya kulingana na mahitaji ya soko, tatu ni kuajiri watumishi na kuwaendeleza kitaaluma.
“Kuanzisha Chuo cha Umahiri cha Mafunzo ya Usafiri wa Anga na Usafirishaji ambacho kinafadhiliwa na Benki ya Dunia. Kuanzisha kituo cha Kikanda cha Mafunzo ya Umahiri wa Usalama Barabarani.
“Sita tuko kwenye mkakati wa kukibadilisha Chuo kuwa Chuo Kikuu cha Usafirishaji kwa ufadhili wa Rais wa China. Saba, Kulipa madeni ya mwaka 2015/16. Nane tunaenda kupitia mpango wa matumizi bora wa ardhi pale Mabibo kwa matakwa ya kuwa Chuo Kikuu.
“Tisa kupanua chuo kwa kuongeza kampasi, ambapo tutakuwa na Kmapasi ya Lindi, Kia Kilimanjaron lakini pia jijini Dodoma, pamoja na hayo tuko kwenye mkakati wa kuanzisha kituo cha Utafiti kwa Usafiri wa Reli.”amesema Mganilwa.

No comments:

Post a Comment

Pages