Kaimu
Kamishna wa Sera Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. William Mhoja akihitimisha
Kongamano la siku mbili la Wanamipango
la mwaka 2019, lililofanyika Jijini
Dodoma.
Na
Farida Ramadhani na Saidina Msangi
WFM,
Dodoma
Wizara
ya Fedha na Mipango imeahidi kufanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na
wataalamu wa mipango ili kuboresha usimamizi wa sera na mipango ya maendeleo ya
nchi.
Hayo
yameelezwa na Kamshina wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. William Mhoja
wakati wa kuhitimisha kongamano la Wanamipango kwa mwaka 2019 lililofanyika
Jijini Dodoma.
Bw.
Mhoja alisema kuwa kongamano hilo limetoa mapendekezo muhimu ambayo yatasaidia
kuboresha upangaji na utekelezaji wa sera na mipango mbalimbali ya maendeleo
nchini.
Aliwashukuru
washiriki wote kwa michango, mawazo na fikra pevu wakati wa kongamano ambayo
itasaidia katika kutatua changamoto mbalimbali zinazohusu taaluma ya mipango.
Naye
Mchumi Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Adam Msumule ,ambaye ni miongoni mwa washiriki
wa kongamano hilo amepongeza waandaaji wa kongamano hilo muhimu kwa ajili ya
kubadilishana uzoefu na kuboresha mipango ya nchi.
Bw.
Msumule alishauri kongamano hilo kufanyika kila mwaka ili kutoa fursa kwa
wataalamu kufanya tathmnini ya mipango iliyopo, iliyotekelezwa na kuona namna ya
kuiboresha.
Kongamano
hilo lililokuwa na kauli mbiu ugharamiaji wa maendeleo, lilitoa fursa kwa washiriki
kujadili mawasilisho mbalimbali ikiwemo vyanzo bunifu vya ugharamiaji mipango
ya maendeleo ya Taifa, Sera, Sheria na mfumo wa kitaasisi unaosimamia
ugharamiaji wa maendeleo nchini.
No comments:
Post a Comment