January 09, 2020

CPA Kikoty: Mikopo ya Halimashauri mkombozi wa wajasiriamali

Mwenyekiti wa EASD, Abdallah Khamis (katikati), akiwa katika picha ya kumbukumbu.










Na Mwandishi Wetu, Kibiti

MAKUNDI ya kina mama vijana na walemavu nchini, wametakiwa kutumia vizuri mikopo inayotolewa na halmashauri mbali mbali kwa ajili ya kuinua maisha yao kiuchumi pamoja na uchumi wan chi.
Wameelezwa kuwa mikopo hiyo kwa makundi hayo ni nafuukwa kuwa haina masharti magumu kama ile inayotolewa na taasisi za kifedha, hali inayowafanya watu wengi kushindwa kupata.
Hayo yalielezwa juzi wilayani Kibiti na CPA.Janeth Kikoty,katika semina ya siku moja  iliyoandaliwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Education Agender for Sustainable Development(EASD),kwa kushirikiana na chama cha wahasibu Tanzania(TAA),ambapo wajasiriamali wa vikundi 16 walishiriki
CPA Kikoty,alisema dhamira ya serikali ni kuona kila mwananchi anafanikiwa hivyo umakini, uaminifu na na kujituma kwa kila anayepata mikopo hiyo kutaiwezesha nchi kufikia uchumi wa viwanda
“Uaminifu ni nguzo kwenu mnaopata mikopo lakini ni vema pia mkaniwekea  mazoea ya kukagua mahesabu yenu kila baada ya kipindi Fulani ili mjue kama mnasogea mbele ama kurudi nyuma”alisema CPA Kikoty.
Katika semina hiyo mkurugenzi wa mipango na elimu wa chama cha wahasibu Tanzania  CPA. Ezekiel Stephen, alisema chama hicho kipo tayari kuwasaidia watanzania mbali mbali katika suala zima la uelewa wa utunzaji wa mahesabu ya fedha kitaalam na kwamba huduma hizo wanazifanya pasipo kuhitaji gharama kutoka katika vikundi vya wajasiriamali
“Sisi TAA tupo tayari kuwasaidieni nyie wajasiriamali kuwapa mafunzo ya namna bora ya kuhifadhi kumbu kumbu zenu za kimahesabu na hili hatulifanyi kwa gharama yeyote pale mtakapokuwa mmejikusanya na kuhitaji elimu hii”alisema CPA.Ezekiel.
Aliongeza kuwa  jambo la muhimu kwa makundi yanayohitaji elimu hiyo ni kufuata utaratibu mzuri wa namna ya kuwafikia  katika maeneo wanayokusudia kupatiwa elimu hiyo
Kwa upande wake Mwenyekiti wa EASD, Abdallah Khamis, alieleza kuwa jukumu kubwa la taasisi yake ni kuhakikisha wanawaunganisha wadau mbali mbali na kuwafikishia elimu mtambuka kulingana na mahitaji husika ya wakati huo
“Tulipata taarifa kuwa mnapewa mikopo na Halmashauri sisi kama taasisi yenye jukumu la kutoa elimu tukawatafuta wenzetu wa TAA na kuwaomba watusaidie wataalam wao kwa ajili ya kuja kuwapa mafunzo haya mnayoyafanya leo”alisema Khamis.
Aliongeza kuwa EASD ni taasisi iliyojipambanua kutoa elimu mtambuka kwa kushirikiana na wataalamu mbali mbali na kwamba huo ni mwanzo wa dhamira yao hiyo.
Awali afisa maendeleo ya Jamii wilaya ya Kibiti  Anthony Nyange alisema  wameshawapatia vikundi 17 mikopo yenye thamani ya sh. Million 40, kupitia mfuko wa maendeleo ya wanawake vijana na walemavu, fedha zilizotoka katika bajeti ya mwaka 2019-20.
Fedha tulizowakopesha leo ni sehemu ya fedha za mfuko wa maendeleo ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu”alisema Nyange.

No comments:

Post a Comment

Pages