January 08, 2020

Karatu Wafurahia kurejea kwa kiwanda cha maziwa kilichohujumiwa

Kiwanda cha Maziwa Karatu Kilichohujumiwa na Wajanja wachache.
 
Na Bryceson Mthias, Karatu
 
WANANCHI wa Wilaya ya Karatu mkoani Arusha, wamezidiwa na furaha baada ya kuwepo kwa tetesi za kurejeshwa kwa Kiwanda cha Maziwa cha Ushirika wa Ayalabe Dairy baada ya fedha zao kuhujumiwa na Wajanja wachache.
Waliofurahishwa na tetesi hizo ni pamoja na wafugaji waliokuwa wakikamua na kuuza maziwa kiwandani na kujipatia kipato wakiwemo wachuuzi na wafanya biashara ya maziwa sehemeu mbalimbali.
Fununu za kurejeshwa kwa Kiwanda hicho katika kazi zake zinadaiwa zinafuatia agizo la Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (Mb), ambaye Novemba 10, 2019 aliagiza viongozi wote wa Chama hicho kukamatwa kutokana na ubadhirifu wa fedha.
Pamoja na kuwepo kwa taarifa za watuhumiwa hao kupata dhamana kutolewa rupango, wananchi hao wamedai wamehemewa na furaha kwa sababu kuna fursa tena ya kuwepo kwa ajira na kukuza kipato chao
Novemba 10, 2019 akiwa kwenye ziara ya kikazi, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (Mb) mara baada ya kusikiliza malalamiko ya wanachama wa Chama hicho kwenye kikao kazi kilichofanyika uwanja wa Chama, aliagiza Jeshi la Polisi, Mkuu wa Upelelezi Arusha kwa kushirikiana na TAKUKURU kuwakamata watuhumiwa.
Waziri Hasunga aliagiza viongozi hao kukamatwa haraka iwezekanavyo kwani dhamira ya Serikali ya awamu ya tano ya kuanzisha vyama vya Ushrika ilikuwa ni kuwanufaisha wananchi kupitia umoja huo.
Waziri Hasunga pia aliagiza kukamatwa kwa viongozi wote wa makampuni yaliyochukua hela kinyume na taratibu za ushirika, na katika hatua nyingine aliagiza mtu mmoja jina linahifadhiwa (Blanka Michael) akamatwe kutokana na kukodisha eneo la Chama cha Ushirika wa Ayalabe Dairy pasipo kufuata utaratibu wa kisheria.
Aidha katika mkutano huo pia Waziri Hasunga aliagiza kuwekwa kizuizini viongozi na wajumbe wa kamati ya usimamizi wa Chama cha Akiba na mikopo cha Ayalabe Majina yao yamehifadhiwa (ni aliyekuwa Mwenyekiti Ndg Lazaro Titus Lazaro  na wajumbe Joseph Bayo na Eudesi Jonas).

No comments:

Post a Comment

Pages