January 05, 2020

MJI WA LAMADI KUWA MIJI BORA BARANI AFRIKA, KUONGOZA PESA ZA KIGENI

Na Andrew Chale, Busega

MJI wa Lamadi uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Mkoa wa Simiyu unatazamiwa kuwa miongoni mwa miji mikubwa Barani Afrika utakaokuwa ukiingiza fedha nyingi za kigeni sambamba na kupokea watalii wengi zaidi kwa mwaka, kutokana na kituo cha michezo cha Maajabu ya Utalii 'Disneyland'.

Hayo yamesemwa mjini hapana  na Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Bernard Kibesse (pichani), wakati akizungumza na Wajasiriamali katika tukio la kukuza na kuendeleza Utalii la Lamadi Utalii Festival, kwenye viwanja vya shule ya Itongo, mjini Lamadi.

Dkt. Kibesse alisema licha ya kuwa Busega ni Wilaya mpya, wanabahati kupata Mkuu wa Wilaya mwanamama na mchapa kazi kutokana na kubuni mambo mengi yenye kuleta tija na fursa za kiuchumi DC Bi. Tan Mwera sambammba na Mkuu wa Mkoa huo, Anthony Mtaka ambao wamekuwa na mbinu za kuja na fursa zenye maendeleo.

Amnapo alieleza kuwa, Lamadi itakuwa ikipokea Watalii  wengi na kwa kuwa mwaka huu mradi huo wa Disneyland unaanza kujengwa, Itakuwa inapokea Watalii zaidi ya 5,000 kwa mwaka ambapo itakuwa chachu katika kuingiza fedha za kigeni.

"Tunampongeza Mkuu wetu wa Mkoa Anthony Mtaka na wasaidizi wake akiwemo DC Tano Mwera na mwaka huu kituo cha Disneyland kinaanza kujengwa hapo eneo la pori la akiba la Kijereshi.
 
Tupopamoja, tutumieni, tuambieni shida zenu tuwafikishie kwa Jemedali Rais, John Pombe Magufuli.
Na kwa kuwaambia tu, Magufuli anaiependa sana Busega, kwani Mkuu wa Majeshi anatoka Busega, Gavana anatoka Busega na wapo wengi wanaotoka Busega mmependelewa kwelikweli, sasa suala sio kupendelewa, tuitumie hiyo nafasi tujiletee maendeleo na kuliletea Taifa maendeleo kupitia Busega hii hii ambayo kwa sasa ni mpya lakini itakuwa ni ya kitofauti hapo baadae." alisema Dkt. Kibesse.

Na kuongeza kuwa: "Nchi zote za Ulaya, Asia, Afrika na kote, watakuwa wanakuja Tanzania, lakini watakuwa wanakuja Busega na mtakuwa mnawaona hapa Lamadi. Nilikuwa huko Marekani Mwezi  wa Sita na wa Saba, watalii karibu 10,000 huwa wanaenda Florida na California   kuangalia michezo ya maajabu ya Disneyland hicho ambacho sasa kinakuja Afrika katika nchi ya Tanzania, Mkoa wa Simiyu Wilaya ya Busega" alisema Dkt. Kibesse.

Pia aliongeza kuwa, Wananchi wa Busega kwa kuwa hawapati fedha za kigeni za kutosha, wametakiwa kutumia fursa za kuwekeza huduma za Kitalii nyingi katika mji huo wa Lamadi.

"Tutumieni fursa za kupata fedha za kigeni 'Dolla',  sisi Lamadi hatuzipati sana Dolla, fursa za mahoteli ni sasa na watakaopata ajira ni wana wa Lamadi, tunakila sababu ya Busega kujidai". alisema. Dkt. Kibesse.

Akielezea  kwa kina juu ya  uchumi wa nchi, matukio kama matamasha na majukwaa ya kiuchumi  katika Utalii, kama ilivyo kwa Lamadi Utalii festival yanafanyika kwa wakati muafaka kabisa kwa nchi kuhimiza ongezeko la fedha za kigeni na Utalii ndio bidhaa inayoongoza kuingiza fedha za kigeni katika nchi hata Wananchi na Rais wanatembea kwa kujidai kwa sababu nchi ina fedha za kigeni za kutosha.

"Nimetoa mfano kwamba akiba iliyopo sasa hivi hata tukasema watanzania wote tukae hatuzalishi, jambo ambalo haliwezekani.

Hatuzalishi tumekaa tu tunakula 'bata' tunakunja nne, tunakunywa zetu soda, kajuisi na kamvinyo kidogo, tunauwezo wa kuimili mikiki yote na uagizaji wa bidhaa kutoka nje kwa miezi sita.

Ebu fikiria hiyo hali, kwamba nchi imelala haifanyi chochote, bado inaweza kuwa 'fanctional' kwa Miezi Sita, sasa hilo sio jambo dogo kwa sababu, moja nchi haiwezi kulala, inaendelea kila siku. kwa hiyo naomba tutumie matamatasha haya kuenzi Utalii wa ndani  na kuvutia watalii wengi zaidi na tytaingiza pesa za  kigeni." alisema Dkt. Kibesse.

Aidha, akizungumzia juu ya uwepo wa benki chache kwenye mji huo wa Kiutalii, alisema kwa muda mrefu Busega ilikuwa na benki moja tu ya Azania, ambayo ipo katika mji wa Lamadi hivyo amewaomba wadau kuja kuekeza huduma hizo.

"Busega ni Wilaya mpya. benki  nyingi huwa zipo kwenye miji na zikijitanua sana zinaenda kwenye Wilaya.

Busega imechelewa sana ndio maana nilipoingia kwenye madaraka haya niliyopo niliizita benki za Kizalendo za CRDB, NMB, POSTA, nikasema haiwezekani nyinyi benki za kizalendo hampo Busega, wameahidi watakuja, kwani benki zikiwa nyingi sehemu fulani ndio chocheo la uchumi hivyo nahimiza mabenki kuja Lamadi ingawa NMB wameanza Nyanshimo.

Lamadi ndio kila kitu maana nchi jirani wanapita hapa na mzunguko wa kibiashara hapa ni mkubwa hivyo natumia wasaha huu mabenki yaje kuwekeza." Alimalizia Dkt. Kibesse.

No comments:

Post a Comment

Pages